MADIWANI WA CHADEMA WAMLALAMIKIA MKUU WA MKOA KWA KUWANYIMA WASISAFIRI


Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama

MADIWANI wa chadema katika manspaa ya Moshi wamelalamikia kitendo cha mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama kuzuia safari yao ya kwenda Kigali nchini Rwanda.

Hata hivyo baadhi ya madiwani hao wamemtaka mkuu wa mkoa kufanya

shughuli zake na kuacha kuingilia mambo ya siasa kwani siyo
yaliyomleta katika mkoa huu wa Kilimanjaro

Mmoja wa madiwani hao Hawa Mushi alisema kuwa kitendo kilichofanyika

ni kama kukandamizwa kwa madiwani hao na kuwa mapato ya ndani
yameongezeka hivyo kulikuwa hakuna sababu ya kuwazuia.

“Mkuu wa mkoa ajue pale tungetumia shilingi milioni 123 tu na tulikuwa

tumekubalianatupewe posho siku tattu tu na siku nne tusipewe hivyo
ndivyo ilivyokuwa’alisema Hawa

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama alipinga kuwapo kwa safari

ya madiwani wa Manispaa ya Moshi ya kwenda katika Jiji la Kigali
nchini  Rwanda kwa madai kuwa bajeti iliyotengwa ya shilingi milioni
123 ni kubwa.

Gama alitoa uamuzi huo wakati akizungumza kwenye kikao cha kamati

ya ulinzi na usalama wa mkoa, ambacho pia kilijumuisha madiwani pamoja
na baadhi ya wakuu wa Idara wa Manispaa ya Moshi, ambapo alibainisha
kuwa safari hiyo haina tija endapo watatumia kiasi kikubwa cha fedha
hizo.

Hata hivyo ieleke kuwa moja ya ajenda waliyokuwa wanaenda kujifunz ani

namana ya kutunza mji na kuufanya kuwa safi wakati huo huo madiwani
hao ndio waliochangia mji wa Moshi kuwa mchafu.

Madiwani hao walibadilisha sheria ya kutunza  mazingira ya kulipa

faini ya shilingi elfu hamsini ikiwa mtu atachafua mazingira hadi
kufika kiasi cha shilingi elfu kumi kwa lengo la kuwasaidia wananchi


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo