Imebainishwa kuwa  moja ya vikwanzo Vinavyokwamisha jitihada za serikali za kuhakikisha kuwa huduma  ya umeme inawafikia wananchi wengi zaidi na kwa kasi kubwa ni gharama kubwa za kuunganisha umeme na kipato cha wananchi wengi wanaohitaji kupata huduma ya umeme. 
Hayo yamebainishwa na waziri wa nishati na madini Prof Sospeter Muhongo wakati akiongea na wadau mbalimbali kutoka mkoani manyara kuhusu mambo ya maendeleo pamoja na mikakati ya kupunguza gharama za kuunganisha umeme kwa wateja iliyofanyika jana katika ukumbi wa white rose mkoani manyara. 
Alisema kuwa gharama hizo zimekuwa ni kikwazo katika azma ya serikali ya kutimiza lengo la asilimia 30 ya wananchi watakaounganishiwa umeme ifikapo mwaka2015. 
Waziri Muhongo aliendelea kusema kuwa kwa kuzingatia chanagamoto hizo serikali kupitia Tanaesco imedhamiria kupunguza gharama za kuunganisha umeme wa njia moja kwa wateja wadogo mijini na vijijini kwa wastani wa kati wa asilimia 30 na 77. 
Alisema kuwa viwango hivyo vya gharama vitaanza kutumika mwezi januari mwaka 2013 ambapo serikali pia imeanzisha utaratibu wa kugharamia miundombinu ya kuwafikishia umeme wateja kwa miradi inayopata ruzuku kutoka mfuko wa nishati vijijini(REF) 
Alieleza kuwa utaratibu huo utatumika kwa wateja watakaokuwa wamefunga nyaya za umeme kwenye nyumba zao katika maeneo ya miradi husika,mpango huo utapunguza gharama za kuunganishiwa umeme kwa wastani  wa asilimia 80% kulingana na idadi ya nguzo na mfumo utakaotumika. 
Pia Waziri wa Nishati na Madini Muhongo  amewataka wakazi wa mkoani manyara wajiwekeze katika ufugaji pamoja na kilimo ili kuweza kujikwamua katika kiuchumi pamoja na umaskini. 
Alisema kuwa asilimia 83% ya wakazi wa mkoa wa manyara wanajishughulisha na ufugaji pamoja na kilimo hivyo waweke mikakati ya maendeleo kupitia ufugaji pamoja na kilimo. 
Alimalizia kwa kusema kuwa ifikapo mwaka 2015 pato litakuwa dola 32.5 bilioni na dira ya maendeleo ya mwaka 2025 Tanzania tutatoka kwenye dimbwi la umaskini.