WATANZANIA ikiwemo watu wenye ulemavu wa aina zote wametakiwa kujitokeza kutembelea vivutio vya taifa ikiwemo kufanya utalii wa kupanda mlima Kilimanjaro ikiwa ni njia moja wapo ya kukuza utalii wa ndani nchini na kuongeza pato la taifa.
Hayo yalibainishwa muongoza watalii katika mlima kilimajaro Abel Beimoja, wakati wa kupokea watalii 12 kutoka nchini Ufaransa ambapo kati yao watu wakiwa na ulemavu wa viungo macho na kutokusikia na kuongea waliopanda mlima huo septemba 10 na kushuka septemba 16kupitia geti la mweka wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro.
Alisema kumekuwa na idadi kubwa ya wageni kutoka nchi nyingi dunia kuja kupanda mlima huo ikiwa ni pamoja na walemavu lakini watanzania walio wazima hawajawahi kupanda mlima huo jambo ambalo ni la kushangaza sana kwa nchi nyingine.
Alisema walemavu kupanda mlima ni jambo la kuvutia katika masikio mwa watu wengi na kwamba ipo haja ya watu wenye ulemavu nchini kujitokeza kufanya utalii wa ndani na kuacha tabia ya kujiona wao hawana dhamani yeyote katika jamii ya watanzania.
Kwa upande wake muhifadhi idara ya utalii mlima Kilimanjaro Steven Moshi aliwataka watanzania kubadilika na kujitokeza kufanya utalii wa ndani ikiwa ni pamoja na kuwasaidia walemavu wanao tamani kupanda mlima huuo kuja na kujione vivutio ndani yam lima huo.
Aidha aliitka jamii kuacha tabia ya kuficha watu wenye ulemavu na kujifunza kutoka nchi nyingine kuwa mlemavu ni mtu wa kawaida na anaweza kufanya kila kitu ikwiwemo kutalii katikavivutio mbalimbli nchini.
 Akizungumza mmoja wa walemavu hao Dominiki Venani  ambaye ni mlemavu wa viungo alisema kuwa ni fahari kubwa kwao kuja kuona mlima huo na kutimiza ndoto yake ya zaidi ya miaka ishirini kabla haja pata ulemavu huo.

