ZAIDI YA VIJANA 30 MKOANI KILIMANJARO WANUFAIKA NA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI

MOSHI

VIJANA zaidi ya 30 katika  kata ya Kahe wilaya ya Moshi vijijini mkoani Kilimanjaro wamenufaika na mafunzo ya ujasiria mali ikiwa ni pamoja na kujiajiri wenyewe katika shughuli za kilimo kutokana  kuwepo kwa changamoto ya ukosefu wa ajira  nchini.

 Hayo yalibainishwa na mkurugenzi mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali la kuwawezesha vijana kujiajiri katika kilimo na ujasiriamali ili kupambana na tatizo la ajira kwa vijana la 'Fumbuka Agro Solution Organization (FASO)' Innocent Mbele ambapo alisema vijana wengi wamekuwa hawana ajira na kujikuta wakiingia katika makundi ya uvutaji wa madawa ya kulevya jambo ambalo limekuwa likipoteza nguvu kazi ya taifa.

 Alisema kutokana na vijana wengi kukosa ajari shirika hilo limeoana ni vema kutoa elimu ya ujasirimali kwa vijana kuhusiana na kilimo kutokana na kwamba ndilo kundi kubwa linalo kabiliwa na changamoto ya ukosefu wa ajira.

 Alisema vijana wengi ni wasomi lakini wamekuwa wakishinda vijiweni na hatimae kujikuta wanakuwa vibaka na kwamba kwa kutoa elimu hiyo ndio njia pekee ya kuwawezesha vijana na kwamba hawana budi kubadilisha fikra za kuajiriwa bali kujiajiri wenyewe ili kuondokana na tatizo la umasikini wa kipato

 Kwa upande wake  Diwani wa kata ya Kahe, Aminiel Kimati alitoa wito  vijana kufanya kazi kwa bidii na kwa na subira kutokana na kamba maendeleo haji kwa hara bali kujituma na kuwa na maadili katika jamii ikiwa ni pamoja na kuacha tabia ya utumiaji wa madawa ya kulevya.

 Mkufunzi wa semina hiyo Mwl.Simon Mushi kutoka chuo cha Kilimo na Mifugo Mwangaria aliwafundisha vijana hao jinsi ya kuchagua mazao bora kulingana na hali ya hewa ya ukanda wao pia jinsi ya kuchagua pembejeo bora za kilimo kama mbegu, mbolea na madawa ya kuuwa wadudu.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo