HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO
WA TANZANIA, MHESHIMIWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE AKIZINDUA AWAMU YA
TATU YA MFUKO WA MAENDELEO YA JAMII (TASAF III) UWANJA WA JAMHURI,
DODOMA, 15 AGOSTI 2012
-
Mhe. Spika;
Mhe. Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar;
Mhe. Steven Wassira, Waziri wa Nchi Ofisi
ya Rais - Uratibu na Mahusiano,
Mhe. Daktari Rehema Nchimbi,
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma;,;
Waheshimiwa Mawaziri na Wabunge;
Mhe. Katibu Mkuu Kiongozi;
Mwakilishi wa Benki ya Dunia: Tanzania,
Uganda na Burundi,
Bwana Philippe Dongier;
Ndugu Peniel Lyimo, Mwenyekiti wa Kamati ya
Taifa ya Uongozi wa TASAF;
Mwakilishi wa Benki ya Dunia;
Wawakilishi wa Ndugu Peniel Lyimo;
wWashirika wetu wangine wa mMaendeleo; ,
Waheshimiwa Viongozi wa Vyama vya Siasa;
Waheshimiwa Wabunge
Viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa nawa
Serikali;
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF;
Wageni wWaalikwa;
Mabibi na Mabwana:;:
Shukrani
Ndugu
Wananchi:
Namshukuru
sana Mheshimiwa Waziri Steven Wassira na Nndugu Ladislaus Mwamanga,
Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) na Kamati
yake kwa kunialika nije kushiriki nanyi kwenye uzinduzi wa Awamu ya Tatu
ya TASAF.Tarehe 30 Machi 2000 tulizindua Awamu ya Kwanza ya Mfuko wa
Kwa kuwa huko tulipotoka tumepata mafanikio ya kutia moyo, naomba nianze
kwa kutoa pongezi na kuwashukuru wote walioshiriki kufanikisha
utekelezaji wa awamu mbili za TASAF zilizotangulia.
Pongezi
Ndugu
Wananchi;
Napenda
kuishukuru kwa dhati Benki ya Dunia na Mwakilishi Mkazi wa Benki hiyo wa
wao hapa nchini kwa kushirikiana na sisi kutekeleza miradi mbalimbali
ya TASAF tangu mwaka 2000. Siku zote Benki ya Dunia imekuwa mwenzetu
muhimu na wa kutumainiwa na hii inasikiliza hoja zetu na kuzingatia
vipaumbele vya sSerikali na wananchi wa Tanzania yetu katika jitihada
zetu za kupambana na umaskini na kujiletea maendeleo. Tunafurahishwa
sana na sera ya kusikiliza vipaumbele vyetu. Jambo hilo Hali hii ndiylo
limetuwezesha sisi kushirikiana nao kubuni mpango huu wa TASAF
unaofadhiliwa na ubia mzuri wa maendeleo kati yetu Serikali na Benki ya
Dunia, , kwa kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo, Serikali zetu
mbili na wananchi wa nchi yetu.
Natoa
ipongezai nyingi kwa sana Kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF, chini ya
uenyekiti imara wa Ndugu Peniel Lyimo, Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri
Mkuu, kwa uongozi wake thabiti wa kusimamia vizuri shughuli za TASAF.
Aidha, nampongeza Katibu Mkuu, Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar kwa usimamizi wake thabiti. Hali kadhalika nNawapongeza pia
viongozi na watendaji katika Halmashauri zote za Tanzania Bara , Afisi
ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa kazi nzuri waifanyayo ya
usimamizi na utekelezaji wa miradi katika awamu iliyotangulia. Bila
uongozi wao thabiti, mafanikio ya Awamu zya Kwanza na Pili yangekuwa ni
ndoto. Kwa namna ya pekee nawapongeza wananchi wote walioitikia wito na
kuchangia kwa hali na mali kufanikisha utekelezaji wa mpango huo wa
kujiletea maendeleo yao wenyewe.
Nitakuwa
mchoyo wa fadhila nisipoipongeza Kamati ya Dkt. Servacius Likwelile,
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, kwa kazi nzuri ya kuandaa Awamu ya
Tatu ya TASAF. Kazi hiyo wameifanya vizuri na kwa umakini mkubwa wahuku
akikishirikiana na Bibi Ida Manjolo na wataalamu wengine wa Benki ya
Dunia. Tunawashukuru sana.
Mabibi na
Mabwana;
Kuna msemo
wa Kiswahili usemao “ukiona vyaelea, ujue vimeundwa”. Na hivi ndivyo
ilivyo kwa TASAF. Siri ya mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa
Awamu ya Pili ni usimamizi mzuri unaofanywa na Menejimenti ya TASAF.
Hivyo napenda kuchukua nafasi hii kuipongeza Menejimenti, Mkurugenzi
Mtendaji, na wafanyakazi wote wa TASAF kwa kusimamia vizuri shughuli na
miradi mbalimbali iliyotekelezwa katika Awamu ya Pili. Ni matumaini
yangu kuwa mtafanya vizuri maradufu katika Awamu ya Tatu tunayoizindua
leo.
Utekelezaji
wa Awamu ya Pili ya TASAF
Ndugu
Wananchi;
Utekelezaji
wa Awamu ya Pili ya TASAF ulikuwa na mafanikio makubwa. Jumla ya
miradi 11,572 imetekelezwa na kati ya hiyo, miradi 4,294 ilikuwa ya
huduma za jamii; miradi 1,405 ya ujenzi na miradi 5,875 ya makundi
maalum. Miradi hiyo imegharimiwa na serikali kwa kushirikiana na
washirika wake wa maendeleo. Serikali imetoa Shillingi bilioni 32.2 na
Benki ya Dunia ilitupatia mkopo wa masharti nafuu wa Shilingi bilioni
322. Washirika wetu wengine walituongezea nguvu kwa kuchangia Shillingi
bilioni 72. Aidha, wananchi wametoa fedha, rasilimali na nguvu kazi
ambazo thamani yake inakadiriwa kuwakwa ujumla ni zaidi ya Shilingi
billioni 20.2.
Miradi ya
Huduma
Miradi ya
Huduma za Jamii imeongeza na/au kuboresha madarasa 5,485; ofisi za
walimu 150; nyumba za walimu 152;, maabara kwenye shule za sekondari
157; majengo ya utawala katika shule za sekondari 20; mabweni ya
wanafunzi 163; vyoo vya wanafunzi 705; madawati 22,946, viti 5,483, meza
4,354; vituo vya afya 63; zahanati 606, nyumba za watumishi wa
zahanati 301, vyoo kwenye zahanati 339, vichomea taka 182; vituo vya
maji 2,198, visima virefu 192, visima vifupi 335 na matanki ya maji 205.
Miradi ya
Ujenzi
Miradi
ya ujenzi, yenyewe imeongeza au kuboresha barabara za vijijini 825;
mabwawa madogo 78; mifumo midogo ya umwagiliaji 289; mifumo ya kuondoa
maji ya mvua barabarani mita 4,593; maghala ya kuhifadhia nafaka 113;
masoko 80; makaravati 901; madaraja ya watembea kwa miguu 64; na, miradi
ya mazingira 608 yenye walengwa 566,938.
Makundi
Maalum
Na miradi
ya makundi maalum imetoa huduma kwa yatima 32,113; wajane 15,205; wazee
17,961; watu wenye ulemavu 7,840; watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI
52,316; na vijana wasio na ajira 36,859. Vilevile, watu 2,083
wamehamasishwa kujikinga na ugonjwa wa UKIMWI.
Mabibi na
Mabwana;
Mafanikio
ya utekelezaji wa Awamu ya Pili ya TASAF hayakuishia hapo. Vikundi
1,778 vyenye wanachama 22,712 vimeundwa kupitia Mpango wa Kuweka Akiba
na Kuwekeza (COMSIP ) katika Halmashauri 44 zilizopo Tanzania Bara,
Unguja na Pemba. Walengwa wote wamepatiwa mafunzo ya kuendesha vikundi
vyao kwa ufanisi pamoja na vifaa. Vilevile, mafunzo ya usimamizi,
utekelezaji bora wa miradi na fani mbalimbali katika ngazi ya vijiji,
wilaya na taifa yametolewa kwa walengwa 27,373.
Serikali
kupitia TASAF imefanikiwa pia kutekeleza Programu ya Kijamii ya
Uhawilishaji Fedha kwa Kaya Maskini kwa majaribio katika Wilaya za
Bagamoyo, Kibaha na Chamwino. Walengwa zaidi ya 13,000 kutoka kaya 6,000
maskini na zilizo katika mazingira hatarishi zilipatiwa ruzuku ya jumla
ya shillingi bilioni moja na nusu. Kaya hizo zimejengewa uwezo na
watoto sasa wanapelekwa kwenye zahanati na vituo vya afya kwa ajili ya
chanjo na kufuatiliwa maendeleo yao.
Aidha,
watoto 1,638 ambao hawakuweza kwenda shule kwa sababu ya umasikini sasa
wameandikishwa na wanakwenda shule. Kati ya wanafunzi hao, 392
wamefaulu kwenda shule za sekondari za kata. Vile vile wazee 4,956
wamewezeshwa kupata huduma za afya na baadhi yao wamejiunga na bima ya
afya ili kupata huduma kwa urahisi na uhakika zaidi. Kufuatia mafanikio
ya haraka ya programu hii, sasa maandalizi yanafanyika ili isambazwe
kwenye Halmashauri zote katika utekelezaji wa Awamu ya Tatu ya TASAF.
Ndugu
Wananchi;
Inafurahisha
kuona jinsi suala la jinsia lilivyozingatiwa katika utekelezaji wa
programu na miradi ya TASAF. Wanaume na wanawake walishirikishwa sawa
sawa katika hatua zote za utekelezaji wa miradi yao. Idadi ya wanawake
katika kamati ya mradi ilipangwa makusudi ili isipungue asilimia 50 ya
jumla ya wajumbe, na idadi ya walengwa wanawake katika miradi ya ujenzi
nayo isipungue asilimia 50. Bahati nzuri akina mama waliokuwa wajumbe
kwenye Kamati mbalimbali wameonesha uwezo mkubwa wa uongozi. Naomba
ushirikishwaji huu uendelee kuimarishwa na akina mama wajitokeze kwa
wingi kushiriki katika usimamizi wa miradi ya TASAF ya Awamu ya Tatu.
Ni wazi
kuwa siri ya mafanikio ya Awamu ya Pili ya TASAF ni ushiriki mzuri wa
wananchi, utayari wao wa kumiliki maendeleo yao wenyewe na moyo wa
kujituma kwao pamoja na uongozi na usimamizi mzuri wa miradi katika
ngazi zote.
Changamoto
Katika Utekelezaji wa Awamu ya Pili
Maendeleo
ya Jamii (TASAF I) kule Mwanhuzi, Wilayani Meatu, Mkoa wa Shinyanga.
Vile vile
tarehe 23 Mei 2005, tulizindua Awamu ya Pili ya Mfuko huu (TASAF II )
kule Wilayani Magu, Mkoa wa Mwanza.
Leo hii
ninayo furaha kubwa kuja hapa Dodoma kuzindua Awamu ya Tatu ya Mfuko wa
Maendeleo ya Jamii (TASAF III).
Tunazindua
Awamu ya Tatu ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii kwa kuwa Awamu ya Kwanza na
ya Pili zimetekelezwa kwa mafanikio makubwa. Hivyo basi, naanza kwa
kutoa shukurani na pongezi zangu za dhati kwa wote walioshiriki
kufanikisha Awamu mbili zilizotangulia na walioshiriki kuandaa Awamu hii
ya Tatu.
Naishukuru
Benki ya Dunia na ninamshukuru Mkurugenzi Mwakilishi wa Benki hii kwa
nchi za Tanzania, Uganda na Burundi, Bw. Philippe Dongier. Kwa hakika
Bw. Dongier anaiwakilisha vyema Benki ya Dunia ambayo siku zote
inasikiliza hoja na kuzingatia vipaumbele vya vita dhidi ya umaskini
vinavyowekwa na Serikali yetu. Mfano halisi ni Mfuko huu wa Maendeleo
ya Jamii - TASAF. Kwa usikivu huo, tumebuni ubia mzuri wa maendeleo
kati ya Serikali yetu, Benki ya Dunia, Wadau wengine wa Maendeleo na
Wananchi.
Napenda
pia, kuwashukuru washirika wengine wa maendeleo ambao wanashiriki Awamu
hii ya Tatu ya TASAF hususan Serikali ya Uingereza kupitia Idara yake ya
Maendeleo ya Kimataifa (DFID), Serikali ya Hispania na Serikali ya
Watu wa Marekani kupitia Shirika lake la Maendeleo ya Kimataifa (USAID).
Ninawashukuru
Wataalam wa Benki ya Dunia na Washirika wengine wa Maendeleo
wakiongozwa na Bibi Ida Manjolo ambao walishirikiana nasi kwa karibu
katika utekelezaji wa Awamu ya Pili ya TASAF na kuandaa Awamu ya Tatu.
Naipongeza
pia Kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF ambayo mwenyekiti wake ni
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Ndugu Peniel M. Lyimo, pamoja na
Kamati ya Maandalizi ya Awamu ya Tatu ya TASAF iliyoongozwa na Naibu
Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Dkt. Servacius B. Likwelile, kwa kazi
nzuri.
Nawapongeza
Viongozi na Watendaji katika Halmashauri zote za Tanzania Bara, Afisi
ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na wananchi wote kwa jumla kwa
usimamizi na utekelezaji wa miradi ya jamii katika awamu zote mbili
zilizotangulia. Wananchi wote waliitikia kwa moyo mkunjufu na ari kubwa
kupokea mawazo ya Serikali katika utekelezaji wa mpango huo wa kujiletea
maendeleo yao wenyewe.
Naipongeza
pia Menejimenti ya TASAF, ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji, Ndugu
Ladislaus J. Mwamanga na wasaidizi wake. Nina imani kuwa wataendelea
kufanya kazi nzuri katika Awamu hii ya Tatu.
Tangu mwaka
2000 TASAF imekuwa ni kichocheo katika jitihada za wananchi kujiletea
maendeleo. TASAF haina miradi; miradi ni ya wananchi. Inachokifanya
TASAF ni kuwawezesha tu wananchi kutekeleza vipaumbele vyao vya
maendeleo.
Awamu ya
Pili ya TASAF iligharimiwa kwa kiasi kikubwa na mkopo wa masharti nafuu
kutoka Benki ya Dunia. Mkopo huo ni kiasi cha Shilingi 322 bilioni
sawa na Dola za Kimarekani 215 milioni. Vilevile kwa utekelezaji mzuri
wa TASAF, kumekuwa na Wahisani na Miradi mingine kupitishia fedha TASAF
zenye jumla ya shilling 72 bilioni sawa na Dola za Kimarekani 45
milioni. Mchango wa Serikali yetu ulikuwa ni Shilingi 32.2 bilioni, na
wananchi walichangia fedha rasilimali na nguvu kazi ambazo thamani yake
ilifikia zaidi ya Shilingi 20.2 bilioni.
Ndugu
Wananchi
Ushiriki wa
wananchi, utayari wao wa kumiliki maendeleo yao na kujituma kwao pamoja
na uongozi na usimamizi mzuri wa kitaifa na halmashauri husika ndio
msingi wa mafanikio ya Awamu ya Pili ya TASAF.
Mafanikio
hayo ni pamoja na :-
1.Jumla ya
miradi 11,572 ilipitishwa na kupewa fedha; miradi 4,294 ikiwa ya Huduma
za Jamii, miradi 1,405 ya Ujenzi na miradi 5,875 ni ya Makundi Maalum.
2.Miradi ya
Huduma za Jamii imeongeza na/au kuboresha madarasa 5,485, ofisi za
walimu 150, nyumba za walimu 152, maabara kwenye shule za sekondari 157,
majengo ya utawala katika shule za sekondari 209, mabweni ya wanafunzi
163, vyoo vya wanafunzi 705, madawati 22,946, viti 5,483, meza 4,354;
zahanati 606, vituo vya afya 63, nyumba za watumishi wa zahanati 301,
vyoo kwenye zahanati 339, vichomea taka 182; vituo vya maji 2,198,
visima virefu 192, visima vifupi 335 na matanki ya maji 205.
3.Miradi ya
ujenzi imeongeza au kuboresha barabara za vijijini 825, mabwawa madogo
78, na mifumo ya kuondoa maji ya mvua barabarani mita 4,593, maghala ya
kuhifadhia nafaka 113, masoko 80, mifumo midogo ya umwagiliaji 289,
makaravati 901, miradi ya mazingira 608 yenye walengwa 566,938 na
madaraja ya watembea kwa miguu 64.
4.Miradi ya
makundi maalum imetoa huduma kwa yatima 32,113, wajane 15,205, wazee
17,961, watu wenye ulemavu 7,840, watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI
52,316 na vijana wasio na ajira 36,859. Vilevile, uhamasishaji juu ya
kudhibiti UKIMWI umetolewa kwa watu 2,083.
5.Vikundi
1,778 vyenye wanachama 22,712 vimeundwa kupitia Mpango wa Kuweka Akiba
na Kuwekeza (COMSIP ) katika Halmashauri 44 na Unguja na PembaWalengwa
wote wamepatiwa mafunzo ya kuendesha vikundi vyao kwa ufanisi pamoja na
vifaa.
6.Mafunzo
ya usimamizi, utekelezaji bora wa miradi na fani mbalimbali katika ngazi
ya vijiji, wilaya na taifa yametolewa kwa walengwa mbalimbali 27,373.
Ndugu
wananchi,
7.Serikali
pia kupitia Awamu ya Pili ya TASAF imefanikiwa kutekeleza Programu ya
Kijamii ya Uhawilishaji Fedha kwa Kaya Maskini kwa majaribio katika
Wilaya za Bagamoyo, Kibaha na Chamwino. Walengwa zaidi ya 13,000 kutoka
kaya 6,000 maskini na zilizo katika mazingira hatarishi zilipatiwa
ruzuku ya jumla ya shillingi bilioni moja na nusu (Sh. 1,500,000,000).
Kaya hizo zimejengewa uwezo na watoto ambao ndiyo walengwa wanapelekwa
kwenye zahanati na vituo vya afya kwa ajili ya chanjo na kufuatilia
maendeleo yao.
8.Aidha,
watoto 1,638 ambao hawakuweza kwenda shule sababu ya umasikini sasa
wameandikishwa na wanakwenda shule. Kati ya wanafunzi hao 392 wamefaulu
kwenda shule za sekondari za kata. Vile vile wazee 4,956 ambao ni
walengwa wamewezeshwa kupata huduma za afya. Pia Kaya za walengwa
zimejiunga na mpango wa bima ya afya ili kupata huduma kwa urahisi na
uhakika zaidi.
9.Programu
hii imekuwa na mchango mkubwa katika kuboresha hali ya maisha ya kaya za
walengwa kwa muda mfupi sana. Mafanikio yake yamefanya sasa programu
hii kusambazwa kwenye Halmashauri zote katika utekelezaji wa TASAF Awamu
ya Tatu. Haya yote yasingewezekana bila ninyi wananchi kukubali kwa
pamoja kushiriki katika kurekebisha hali ya uchumi wetu, kwa kuwa
muhimili mkuuwa maendeleo katika ngazi ya jamii.
Ndugu
wananchi,
Kwa kuwa
TASAF imepanua uwigo wa kuwafikia walengwa masikini katika makundi
mbalimbali ndani ya Tanzania Bara na Zanzibar na uzoevu wao wa zaidi ya
miaka kumi na mbili; ni dhahili kuwa ni chombo pekee cha serikali chenye
uwezo wa kutekeleza vizuri Mpango wa Kitaifa wa Kinga ya Jamii (
National Social Protection Framework)
Awamu ya
Pili ya TASAF imeimarisha uwajibikaji katika ngazi zote kwa kuhakikisha
kuwa fedha zote zilizotengwa kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli
mbalimbali zinatolewa taarifa na wadau wote wanajulishwa mapato na
matumizi yake. Kamati za usimamizi wa miradi ziliwajibika kutoa taarifa
za utekelezaji hatua kwa hatua na matumizi ya fedha.
Suala la
jinsia katika utekelezaji wa miradi lilizingatiwa, na kuonekana wazi
kuwa ni jambo la haki na la manufaa kila palipokuwa na mradi
unaochangiwa na TASAF. Wanaume na wanawake walishirikishwa sawa sawa
katika hatua zote za utekelezaji wa miradi yao. Idadi ya wanawake katika
kamati ya mradi ilipangwa kwa makusudi isipungue asilimia 50 ya jumla
ya wajumbe, na idadi ya walengwa wanawake katika miradi ya ujenzi nayo
isipungue asilimia 50. Lengo ni kuhakikisha kuwa kipato kisichopungua
asilimia 50 kinaelekezwa kwa walengwa ambao ni wanawake. Matumaini
yangu ni kuwa uwezo waliouonyesha wanawake waliokuwa kwenye kamati hizi
utawasukuma wengi wao kuomba uongozi katika ngazi mbalimbali.
Ndugu
wananchi;
Pamoja na
mafanikio hayo ya kutia moyo, Wakati wa utekelezaji wa Awamu ya Pili
ulikabiliwa na changamoto ya TASAF kumekuwepo na changamoto mbalilmbali.
Changamoto hizo ni pamoja na uhaba wa fedha kutokutosheleza kukidhi
wezo wa Mfuko kutokidhi mmahitaji ya wananchi; uwezo mdogo wa kusimamia
miradi katika ngazi mbalimbali za uongozi; na ya wananchi ambayo ni
mengi, ukosefu wa huduma kwenye baadhi ya vituo vya kutolea huduma kama
zahuhaba wa watumishi katika vituo vya kutoa huduma. Bahati nzuri
serikali na uongozi wa TASAF unazitambua changamoto hizo na tumejipanga
vizuri kukabiliana nazo katika Awamu hii ya Tatu tunayoizindua leo.
Awamu ya
Tatu ya TASAF
anati,
vituo vya afya na masoko vilivyotokana na miradi kutokana na sababu
mbalimbali kama vile uhaba wa watumishi.
Changamoto
nyingine ni pamoja uhaba wa fedha za utekelezaji wa shughuli za kujenga
uwezo, wigo mdogo wa utekelezaji wa jitihada nyingine, kama vile Mpango
wa Jamii wa Uhawilishaji Fedha kwa Kaya Maskini, Mpango wa Jamii wa
Kuweka Akiba na Kuwekeza, uansishwaji wa Taasisi za Maendeleo ya Jamii
katika sehemu za mijini.
Kadhalika
ilijitokeza changamoto ambapo baadhi ya wanasiasa walipotosha dhana ya
kuanzishwa kwa TASAF na pia kutokuwepo mfumo wa uendelevu thabiti wa
kutekeleza TASAF kwa kutegemea rasilimali za ndani.
Mabibi na
Mabwana;Ndugu wananchi
Kufuatia
mafanikio katika utekelezaji wa Awamu mbili zilizotangulia na pia katika
kukabiliana na changamoto zake, Serikali imeamua kuanzisha Awamu ya
Tatu ya TASAF itatekelezwa kwa miaka kumi, katika vipindi viwili vya
miaka mitano mitano. ambapo Muondo wake umezingatia kupata ufumbuzi wa
chanamoto zilizopatikana na hivyo ambayo itatekelezwa katika kipindi
cha miaka kumi nchi nzima kwa Awamu mbili za miaka mitano mitano.
Tunategemea
Awamu hii
ya Tatu ya TASAF itatoa mchango mkubwa katika kufikia nalenga
kuchangania kufikiwa malengo yetu yaliyomo kwenye ya D Dira ya Maendeleo
ya Taifa 2025, Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano, Mkakati wa Pili wa
Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini (MKUKUTA II) na Mkakati wa Pili wa
Kukuza Uchumi Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Zanzibar (MKUZA II) na
Mpango wa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mita. Tutaweka mkazo zaidi
katika miradi ya huduma za elimu, afya na maji nay a kuondoa umaskini wa
kipato. no kwa kuwekeza katika kuendeleza rasilimali watu miongoni mwa
kaya maskini na zilizo katika mazingira hatarishi. Kupitia utekelezaji
wa Awamu ya Tatu ya TASAF tunatarajiainatarajiwa kuwa kaya
nyingimaskini maskini zitapiga hatua na kutoka kwenyekuanza kutoka
katika umaskini namaisha ya utegemezi. hatimaye kuwa na mchango katika
kukuza uchumi na kuondokana na utegemezi.
Ili
kutekeleza miradi ya Awamu ya Tatu ya TASAF, jumla ya Shilingi bilioni
408 zitahitajika. Fedha hizo zitatolewa na serikali yetu, Benki ya Dunia
na washirika wengine wa maendeleo. Serikali itatoa Shillingi bilioni
45; Benki ya Dunia itachangia Shillingi bilioni 330; Hispania itatoa
Shillingi bilioni 9; Uingereza Shillingi bilioni 24; na Marekani
Shillingi bilioni 1.4. Kama ilivyokuwa kwa Awamu zilizotangulia,
tunawategemea sana wananchi kutuunga mkono na kuchangia kwa hali na
mali. Mafanikio ya Awamu hii yatategemea sana mchango wa wananchi katika
maeneo husika.
Ahadi na
Wito kwa Wananchi
Ndugu
wananchi;
Tunapenda
kuahidi kuwa tutaendelea kushirikiana na wananchi wote ambao wanaonesha
dhamira ya dhati ya kupambana na umaskini na kujiongezea
Kwa
ushirikiano wenu wananchi, TASAF imetekelezwa vizuri sana na matunda
yake yapo wazi, na kwa vile mmeendelea kuiunga mkono Serikali yenu ya
CCM katika kutekeleza Mwelekeo wa Sera zake za Miaka mitano (2010-2015)
zinazohimiza mageuzi ya kiuchumi na uwezeshaji wananchi, serikali
imetenga fedha tena na kupata mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya
Dunia na washirika wengine wa maendeleo ili kutekeleza Awamu ya Tatu ya
TASAF.
Bodi ya
Wakurugenzi wa Benki ya Dunia iliridhia na kupitisha utekelezaji wa
Awamu ya Tatu ya TASAF tarehe 29 Machi, 2012. Mkataba kati ya Benki ya
Dunia na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulisainiwa tarehe
15 Juni 2012. Na idhini ya kuanza kutumia fedha hizo tayari
imeshatolewa.
Awamu ya
Tatu ya TASAF inatarajiwa kugharimu Shilingi 408 Bilioni sawa na Dola za
Kimarekani 272 Milioni kwa mchanganuo ufuatao:
1.Benki ya
Dunia itachangia shilingi 330 bilioni (USD 220 milioni),
2.Serikali
ya Hispania itachangia Shilingi 9 bilioni (USD 6 milioni)
3.Serikali
ya Uingereza kwa kupitia Idara ya Serikali ya Uingereza ya Maendeleo ya
Kimataifa(DFID) itachangia Shilingi 24 bilioni (USD 16 milioni)
4.Serikali
ya Watu wa Marekani kupitia Shirika la Marekani la Maendeleo ya
Kimataifa (USAID) itachangia Shillingi 1.44 bilioni ( USD 900,000)
5.Serikali
ya Tanzania itachangia sh.45 bilioni (USD 30 milioni)
Ndugu
wananchi
Utekelezaji
wa Awamu ya Tatu ya TASAF unategemewa kuwa na changamoto zifuatazo:
1.Upatikanaji
wa raslimali fedha za kukidhi mahitaji halisi ya walengwa. Jitihada za
kupata rasilimali zaidi ziendelee na Wadau wa Maendeleo watoe
ushirikiano zaidi hasa wale ambao wameonyesha nia ya kushiriki katika
kuchangia mfuko huu.
2.Kujenga
uwezo mapema wa kusimamia na kutekeleza kwa wakati uhawilishaji wa fedha
kwa walengwa. Mpango wa kujenga uwezo wa watekelezaji katika ngazi
mbalimbali upewe kipaumbele. Ufuatiliaji na tathmini vifanyike ili
kubaini mapungufu mapema iwezekanavyo.
3.Uwezo wa
kusimamia utekelezaji miradi kwa ufanisi na kwa wakati. Ngazi zote
zinazohusika na utekelezaji zishiriki kikamilifu katika kuhakikisha
usimamizi wa utekelezaji unafanyika ipasavyo. Aidha, utekelezaji
ufanyike kwa awamu kuzingatia uwezo unavyojengwa.
4.Kusimamia
uendelevu wa rasilimali na vituo vya kutolea huduma vilivyotokana na
miradi iliyotekelezwa na wananchi. Wataalamu kutoka halmashauri husika
na Viongozi katika maeneo ya utekelezaji wawezesha jamii kuwa na mipango
endelevu ya uendeshaji.
5.Usimamizi
wa fedha zitakazotolewa kutekeleza miradi inayochangiwa na TASAF
utahitaji uwepo wa udhibiti mkubwa katika ngazi zote. Kazi hiyo nayo
ifanywe kuanzia sasa na kwa kipindi chote cha utekelezaji.
Ndugu
wananchi,
Leo
tunapozindua Awamu ya Tatu ya TASAF napenda tujikumbushe kuwa historia
yetu ya vita dhidi ya umaskini imetufundisha mambo kadhaa:
Kwanza,
sera nzuri, mipango mizuri na nia njema peke yake havileti
maendeleo.
Pili, fedha
za Serikali, mikopo au wahisani peke yake hazileti
maendeleo.
Tatu, ipo
tofauti kubwa kati ya kutamani maendeleo na kuwa tayari
kutoka
jasho kutafuta maendeleo.
Baada ya
miaka 50 ya Uhuru sasa nadhani tumeelewa kunahitajika nini ili maendeleo
yaje kwa kasi ya kutosha kuweza kupunguza na hatimaye kuondoa umaskini
kabisa.
Hatua ya
kwanza ya maendeleo ni mtu kutoridhika na hali duni ya maisha yake; ni
kujenga tamaa na wivu wa maendeleo na kuchukia hali ya umaskini.
Hatua ya
pili ni mtu kuamua kwa dhati kutafuta maendeleo kwa jasho
lake, na
inapobidi kwa kushirikiana na wenzake wanaochukia umaskini kama yeye.
Hatua ya
tatu ni mtu kupima uwezo alionao – uwezo wa fedha na wa mali nyingine;
uwezo wa akili na maarifa; na uwezo wa nguvu za kufanya kazi na kubuni
mbinu za kutumia ili kuboresha hali yake ya maisha na hali ya jamii yake
kwa ujumla.
Hatua ya
nne ni kutekeleza kwa kadri ya uwezo wake mbinu za maendeleo
alizozibuni, au zilizobuniwa na jamii yake.
Hatua ya
tano ni kuomba msaada kwa yale mambo yaliyo nje ya uwezo wake, ikiwemo
msaada wa fedha, msaada wa vifaa, au msaada wa elimu na utaalamu.
Mfuko huu
wa Kuongeza Uwezo wa Wananchi katika Maendeleo ni jitihada nyingine ya
Serikali kuwasaidia wale wananchi ambao wamepitia hatua zote hizo za
kutafuta maendeleo, yaani tayari wameonyesha chuki yao dhidi ya
umaskini, wameamua kwa dhati kuondokana na umaskini kwa kuongeza kkipato
chao. Kipato cha mtu kinapoongezeka watoto wake watahudhuria masomo na
kupata huduma bora za afya. Wazee na akina mama nao watapata huduma bora
za afya. Lakini kipato hakiwezi kuongezeka kama mtu hataki kufanya
kazi, hataki maendeleo, na hataki kujishughulisha na kitu chochote.
Maisha bora kwa kila mMtanzania yatapatikana kama tutafanya kazi kwa
bidii na maarifa. Inawezekana, kila mtu atimize wajibu wake.
kaya ili
watoto wahudhurie masomo na kwenda kliniki kupata chanjo na huduma
zingine za afya. Vile vile ongezeko la kipato litawezesha akina mama
wajawazito na wazee kupata huduma zote muhimu za afya.
Hivyo ndugu
zangu natoa wito kwa wananchi wote watumie vizuri fursa hii murua ya
TASAF. Tushirikiane na uongozi wa TASAF kubuni miradi itakayotuletea
maendeleo ya haraka, miradi itakayoboresha huduma za jamii. Tushirikiane
nao kusimamia utekelezaji wa miradi hiyo. Tuhakikishe kuwa tunafuata
maelekezo ya wataalam na viongozi wetu katika ngazi mbalimbali.
Tuwafichue wabadhirifu wa fedha za miradi ya TASAF na wale wote
wanaotumia vibaya rasilimali za miradi. Daima tukumbuke kuwa miradi hii
ni kwa ajili yetu sisi pamoja na watoto wetu, ndugu zetu na jamaa zetu.
Tukifanya hivi nina imani tutakuwa na msingi imara wa kujenga taifa
linaloendelea na hatimaye kushinda vita dhidi ya adui watatu wa
maendeleo: umaskini, njaa na magonjwa.
Rai kwa
Washirika wa Maendeleo na Viongozi wa TASAF
Mabibi na
Mabwana;
Natumaini
washirika wetu wa maendeleo wataendelea kuunga mkono juhudi zetu hizi
za kuondoa maadui watatu wa maendeleo. Wamekuwa wakifanya hivyo tangu
tulipoanzisha Mfuko huu wa TASAF na nina imani wataendelea. Msaada wao
utasaidia sana kufikia malengo yetu tuliyojiwekea katika utekelezaji wa
Awamu hii.
Nawaomba
pia viongozi wa TASAF, Kamati ya Taifa ya Uongozi, Menejimenti na
Mkurugenzi Mtendaji waongeze ufanisi na maarifa katika utendaji wao.
Waongeze usimamizi wa fedha na rasilimali, wajenge uwezo wa kusimamia
utekelezaji wa miradi katika ngazi mbalimbali, na wabuni vyanzo vingine
vya kupata fedha za kuendeleza miradi. Naamini wataweza.
Mwisho
Mheshimiwa
Waziri;
Wageni
waalikwa;
Mabibi na
Mabwana;
Kabla ya
kumaliza hotuba yangu naomba nitoe shukrani za dhati kwa Mhe. Benjamin
William Mkapa, Rais wa Awamu ya Tatu kwa kubuni wazo hili jema ambalo
manufaa yake tunayaona. Baada ya kusema hayo, sasa nipo tayari kufanya
kazi iliyonileta hapa Nazindua Awamu ya Tatu ya Mfuko wa Maendeleo ya
Jamii kwa matumaini makubwa kuwawamba sasa Watanzania sasa tumeupata
ufunguo wa maendeleo yetu sote. Napenda kutamka kwamba Awamu ya Tatu ya
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii, (TASAF) umezinduliwa rasmi leo. Nawatakia
kila la heri na mafanikio katika utekelezaji wake.
Asanteni
sana kwa kunisikiliza.kwa kutumia fursa ambazo mageuzi ya uchumi, na
usimamizi bora wa uchumi, umeweka mbele yetu.
Kwa pamoja
tutafanya mengi. Na kwa mradi huu wa TASAF, ukichanganywa na miradi
mingine, na utaratibu huu wa kushirikisha wananchi katika shughuli za
kupunguza umasikini, ninaamini Watanzania wote tutakuwa na msingi imara
wa kujenga taifa linaloendelea na hatimaye kushinda vita dhidi ya
umaskini.
Na sasa
natangaza kuwa nimezindua rasmi Awamu ya Tatu ya Mfuko wa Maendeleo ya
Jamii (TASAF III).
Ahsanteni sana kwa kunisikiliza.
