Siha
Mjumbe wa Mkutano Mkuu
wa umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Kilimanjaro,
bwana
Meijo Laiza ametangaza kugombea nafasi ya Ujumbe Halmashauri Kuu ya CCM
taifa(NEC) kupitia Wilaya ya Siha.
Akizungumza na Radio
Kili fm katika zoezi la kuchukua fomu ya kugombea nafasi mbalimbali
ndani ya
chama, Laiza amesema kilichomsukuma kuchukua fomu kugombea nafasi ya juu
ya
kiuwakilishi ndani ya Chama ni kiu ya kutaka kurudisha imani ya wananchi
kwa
CCM na kuwasilisha sauti ya Vijana wa Siha katika Vikao muhimu vya
chama.
Amesema kwa miaka mingi
Wilaya ya Siha imekosa uwakilishi mzurio wa vijana katika vikao muhimu
ya Chama
na kutokana na kuwa kijana ameamua kuchukua fursa ya kuwawakilisha
vijana
wenzake.
Laiza amesema kuwa
pamoja na Wananchi kumuomba kuwania nafasi za juu katika Chama, kwa muda
mrefu
kumekuwa na ulegevu katika kutekelezwa kwa ilani ya Chama cha Mapinduzi
(CCM)
na ahadi za Chama kitu ambacho kimechangia kwa Mkoa wa Kilimanjaro
ambayo hapo
zamani ilifahamika kuwa Ngome ya CCM kutekwa na Vyama vya Upinzani.
Wengine waliochukua fomu
za kugombea nafasi ya UJumbe Halmashauri Kuu (NEC), ni Naibu Waziri wa
TAMISEMI
na Mbunge wa Siha, Aggrey Mwanry na kada wa CCM Joha Mtawazo.