
Ni miezi kadhaa imepita sasa tangu kifo cha one of the best actor ever
in Tzee film industry kwa jina la Steven
Kanumba kitokee.
Na Mama mzazi wa Marehemu Steven Kanumba
kusema kampuni ya Kanumba The Great itakuwa inafanya kazi chini
ya usimamizi wa Seth Bosco na Abela au Mrs Bile ambae ni dada yake na
Marehemu Steven Kanumba ambae Kanumba ndio alikua anamfata kwa
kuzaliwa.
Latest infoz nikuwa company hiyo imeshakamilisha movie mpya kwa jina la
“Malaika” ikiwa imeshirikisha wasanii km Rose Ndauka, Abdalah Mkumbila, Seth
Bosco na Kijana Rammy Galis
ambaye anatarajiwa kuwa Kanumba part 2 kutokana na muonekano wake
kufanana na The late Steven Kanumba.
Filamu hii inatarajiwa kuwaburudisha mashabiki wa Kanumba na itasambazwa
na Steps Entertainment LTD , kaa mkao wa kula kijipatia Copy
yako pindi itapokuwa madukani.