ZOEZI la Sensa na Makazi mkoani Mara
linaendelea Vizuri mpaka sasa licha ya kuwepo
kwa kasoro ndogo tangu kuanza kwake hapo Siku ya Jumamosi usiku chini
nzima.
Mratibu wa Takwimu mkoani Mara Bw. Ramadhani Mbega
amesema kuwa mpaka sasa taarifa alizozipata kutoka sehemu mbalimbali
mkoani
Mara zinaashiria zoezi hilo kwenda vizuri.
Amesema Matatizo madogo ambayo yalikuwepo kama
vifaa,picha kwa makarani kama utambulisho yametatuliwa na hivyo zoezi
zima
kuendelea kama lilivyopangwa.
Aidha katika maeneo ya Mbugani na Visiwani,Bw Mbega
amesema kuwa zoezi hilo limeendelea Vizuri kutokana na maandalizi
yaliyokuwe
hapo awali.
Mbali na maeneo hao Bw. Mbega amesema kuwa kuna
baadhi ya maeneo ambapo viongozi wa vijiji na vitongoji walikuwa
wanalalamika
juu ya maalipo yao na kuongeza kuwa malipo hayo yanatolewa kwa awamu
kama
ilivyoagizwa
Kwa sababu hiyo Mratibu huyo wa Takwimu mkoa wa Mara
amewataka wananchi wote wa Mkoa wa Maraa kuendelea kujitokeza katika
zoezi hilo
kwani kwa kufanya hivyo wataisaidia Serikali katika kupango mipango ya
Maendeleo
kwa wananchi.