Manyara.
WANACHAMA watatu
wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) Mkoani Manyara wamejitokeza kuchukua fomu za kugombea
nafasi ya
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM) mkoani humo.
Taarifa hiyo
imetolewa na kaimu
Katibu wa UVCCM mkoani Manyara Raphael Sumaye wakati akiongea na
waandishi wa
habari mkoani Manyara.
Aidha Sumaye
aliwataja vijana hao
ambao waliojitokeza kugombea nafasi hiyo ya Uenyekiti ni Aloyce
Pasian,Kandemeda Massala na Regina Ndege.
Aliendelea
kuwataja wagombea wa
nafasi moja ya Ujumbe wa Baraza la UVCCM Taifa ni Rajabu Dago,Valleria
Juwali
na Kombo Vitabado huku Amani Mshamu,Lendukus Keia na Peter Nyigu
wakigombea
ujumbe wa halmashauri Kuu ya CCM mkoa.
Pia kaimu Katibu
huyo wa UVCCM
mkoani Manyara aliwataja wagombea wawili waliogombea nafasi moja ya
ujumbe wa
Mkutanao mkuu wa CCM mkoani humo ni Blandina Michael na Paschalina
Emmanuel.
Vile vile
aliwataja wagombea wawili
wa nafasi moja ya ujumbe wa Umoja wa Wanawake (UWT) mkoani humo ni
Rachel Wade
na Zahra Goda na mgombea mmoja Emialia Alfred amegombea nafasi moja ya
jumuiya
ya wazazi ya mkoa huo.
“Hata
hivyo,nimefarijika mno kutokana
na mwitikio wa vijana wa CCM waliojitokeza kwa ajili ya kugombea nafasi
mbalimbali za UVCCM mkoani Manyara kwa uchaguzi unaotarajiwa kufanyika
hivi
karibuni,” alisema Sumaye.
Alisema kuwa
Agosti 14 Kamati ya
Siasa ya mkoa chini ya Mwenyekiti wake Lucas Ole Mukus inatarajia
kupitia
majina haya kabla ya kuyapeleka kwenye ngazi ya Taifa ambao ndiyo wenye
nafasi
ya mwisho ya kupitisha majina haya.
Aliongeza kuwa
Kamati ya
Utekelezaji ya UVCCM mkoani humo chini ya Mwenyekiti wake Janes Darabe
ambaye
hatagombea tena nafasi hiyo kutokana na umri mkubwa imeshayapitia majina
hayo
na kuyapeleka ngazi husika.

