Arusha,
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uganda Hillary Onek
ameshauri
Mamlaka za Magereza Afrika Mashariki (EAC) kubadilishana uzoefu na
desturi
zilizo njema katika usimamizi wa adhabu za vifungo kwa wafungwa.
‘’Tunatakiwa kuhakikisha kwamba magereza yetu ya
kikoloni
yanaangalia utu na haki kwa wafungwa kama maadili yake muhimu,”alieleza
waziri
wakati akiuuhutubia mkutano wa siku tatu wa wakuu wa Magereza na Vyuo
vya
Mafunzo mjini Kampala ambao ulimalizika juzi, kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa
na Sekretarieti ya EAC.
Alisema kuwa nchi za Afrika Mashariki zinatakiwa
kuweka
msisitizo kwenye maboresho katika magereza ili kuwawezesha wafungwa
wanapomaliza vifungo vyao kujengeka na kuwa werevu.
‘’Tunauwezo na lazima tusiruhusu wafungwa
waliobadika kuwa
wazalishaji wa wahalifu sugu katika jamii mara wanapoachiwa kutoka
gerezani,”
alisisitiza.
Alisema nchi za Afrika Mashariki ziepuke ukoloni
katika
magereza ambapo Waafrika walikuwa wanadhalilishwa utu wao.
“Magereza yetu baada ya uhuru lazima yawe na sura
ya utu,
utaalam na yatoe malengo yaliyo kusudiwa,” Waziri Mganda alifafanua, na
kuongeza kuwa magereza yasiwe mahali pa mapigano, kufungiwa na kutendewa
unyama
kwa wafungwa.
Naibu Katibu Mkuu wa EAC, anayeshughulikia
Shirikisho la
Kisiasa, Dk.Julius Rotich, alisema magereza na vyuo vya mafunzo
vimejumuishwa
katika mipango ya ulinzi na usalama katika kanda kwa nchi wanachama wa
EAC.
Dk.Rotich alisema hii ilikuwa muhimu kwa EAC,
akisema
itachangia katika kufanikisha utekelezaji wa utaratibu wa soko la
pamoja, hatua
ya pili ya mwingiliano wa kikanda.
Hatua ya kwanza ya mtangamano ilikuwa Umoja wa
Forodha
ambayo ilianza kutumika Januari 2005. Nchi wanachama sasa yanajadiliana
kufikia
Umoja wa Sarafu.
Hata hivyo, Naibu Katibu Mkuu huyo alibainisha kuwa
sekta
ya Ulinzi na Usalama bado inakabiliwa na changamoto katika ufadhili.
‘’Hii haina matumaini mazuri katika mtangamano
imara.
Wakati Sekretarieti ya EAC na nchi wanachama zikijaribu kutafuta njia
mbadala
za ufadhili wa shughuli za kikanda, mamlaka za Magereza zitatakiwa kila
mara
kuunga mkono mikakati iliyopangwa,” alisema ofisa huyo wa EAC.
Mwanyekiti wa Mkutano, Daniel Mutua, kutoka Kenya,
alisititiza huduma za kisasa na zinazofaa kwenye magereza katika kanda
ili
kutimiza malengo ya mtangamano wa EAC.
‘’Mafunzo na uandaaji bora wa mamlaka katika
magereza
utawezesha kutoa matunda yaliyokusudiwa,” aliseama. Wajumbe pia
walitembelea
magereza mjini Kampala.
