Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr. Christine Ishengoma
Vyombo vya habari
Mkoani Iringa
vimeshauriwa kuendelea kuhamasisha zoezi la Sensa ya Watu na Makazi ili
liweze
kufanikiwa katika Mkoa wa Iringa na taifa kwa ujumla.
Rai
hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Christine Ishengoma muda
mfupi
baada ya kuhesabiwa katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi lililoanza
usiku wa
Kuamkia leo nchini kote.
Dkt.
Christine amesema kuwa zoezi hilo vimeanza vizuri na mdadisi ameonekana
kubobea
katika kazi hiyo. Aidha, amewamwagia sifa wakufunzi na wadadasi kwa
jinsi
walivyoonesha juhudi katika kufundisha na kujifunza mambo mbalimbali
yanayohusu
uelewa wa zoezi zima la Sensa ya Watu na Makazi.
Mkuu
wa Mkoa wa Iringa ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya Sensa ya Mkoa
amevipongeza vyombo vya habari vya Mkoa wa Iringa kwa weledi katika
kuhamasisha
zoezi hili.
Amesema uhamasishaji ni muhimu sana katika kutoa hamasa kwa
kazi ya
Sensa ili asitokee mtu ambaye atakuwa hakupata taarifa na elimu juu ya
umuhimu
wa Sensa na kuhesabiwa.
Aidha, ametoa wito kwa vyombo hivyo kuendelea na
uhamasishaji huo kwa kipindi cha wiki nzima ili kulifanikisha zoezi hili
katika
Mkoa wa Iringa. “kufanikiwa kwa zoezi hili Mkoani Iringa sit u kutakuwa
na
manufaa kwa Mkoa wetu, bali kwa nchi nzima na jambo hili litafikiwa pale
tu
wananchi wote watakapokuwa wameelewa umuhimu wa zoezi hili na kushiriki
katika
kulifanikisha” alisisitiza Dkt. Christine.
Akiongelea
matukio
yasiyo ya kawaida katika zoezi hili, Mwenyekiti wa Kamati ya Sensa Mkoa
wa Iringa amesema kuwa zoezi hilo limeanza katika hali ya utulivu mkubwa
na
hakuna tukio lolote lisilo la kawaida lililotokea na kuripotiwa.
Aidha,
amewata
wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa makarani wa Sensa pindi
watakapopita
katika maeneo yao na kujibu kwa usahihi maswali watakayokuwa wakiulizwa.
Katibu
Tawala Mkoa wa Iringa, Gertrude Mpaka, akitoa maoni yake baada ya
kuhesabiwa
asubuhi ya leo amesema kuwa kazi ya kuhesabu na kuhesabiwa ni jukumu la
kila
mtanzania pasipo kujali mipaka ya aina yoyote.
Amesema kila mtanzania
anayo
haki ya kuhesabiwa katika Sensa hii ili kuhakikisha Serikali yake
inapata
taarifa sahihi kwa ajili ya kupanga mipango ya maendeleo kwa wananchi
wake.
Mpaka
amesema “miongoni mwa michango ya wananchi katika jitihada za kujiletea
maendelea kwa kushirikiana na Serikali yao ni pamoja na kushiriki katika
Sensa
ya Watu na Makazi ya mwaka huu”. Amesema zipo njia mbalimbali za
kushiriki
katika shughuli za maendeleo katika kipindi hiki kutoa taarifa sahihi ni
jukumu
namba moja ili kuiwezesha Serikali kupata takwimu sahihi.
Sensa
ya Watu na Makazi inafanyika kwa mara ya tano nchini ikiongozwa na
kaulimbiu
isemayo ‘Sensa kwa Maendeleo, jiandae kuhesabiwa’ ipo katika siku yake
ya
kwanza nchini kote na itaendelea kwa siku saba ili kuhakikisha kila
mwananchi
anahesabiwa mara moja tu.