Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Ofisa kutoka Ofisi ya Takwimu ya Taifa, Radegunda Maro, wakati ofisa huyo alipofika nyumbani kwa Makamu akiwa na Karani wa Sensa na msimamizi wake kutoka Kituo cha Oysterbay, kwa ajili ya kukamilisha zoezi la Sensa, leo asubuhi Agosti, 26, 2012. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijiandaa kujibu maswali kutoka
kwa Karani wa Sensa, Happyness Masaka (kulia) ikiwa ni sehemu ya
kukamilisha zoezi hilo la Senza ya watu na Makazi, lililoanza leo nchini
kote, ambalo litadumu kwa siku saba.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Karani wa Senza,
Happyness Masaka, baada ya kukamilisha zoezi la kujibu maswali husika
katika zoezi hilo, leo asubuhi nyumbani kwake Oysterbay, jijini Dar es
Salaam. Kulia ni Msimamizi wa Sensa wa Kituo cha Oysterbay, Daria
Kailembo (kushoto) ni Ofisa kutoka Ofisi ya Takwimu ya Ttifa, Stanley
Mahembe


