Taarifa hiyo imetolewa na waziri wa fedha Dkt. Wilium
Mgimwa kwa waandishi wa habari katika kijiji cha Kidamali Mkoani Iringa baada
ya mkutano wa hadhara baada ya wavijiji katika wilaya ya Iringa vijijini kutaka
serikali imalize kero ya kukosa simu za kiganjani
Dkt. Mgimwa amesema serikali inaendelea kutafuta mkandarasi
wa kufanya uchambuzi ili kuona namna serikali itakavyoshirikiana na wawekezaji
kufanikisha utekelezaji wa mpango huo wa kusambaza huduma za simu kila sehemu
nchini
Katika mikutano hiyo wananchi wa viijiji hivyo walidai
huduma hiyo ya simu za mkononi ni ya muhimu kwa sasa hivyo serikali inatakiwa
kuharakisha
Katika kijiji cha Ikungwe na kijiji cha Mfyambe pia wakazi
hao hawakusita kutoa kero zao ambao pia zilijibiwa na Mh. Waziri ikiwemo
ulanguzi wa pembejeo za kilimo hasa mbolea za ruzuku
