Jeshi la polisi mkoani Katavi kwa kushirikiana na askari wa
TANAPA katika hifadhi ya Katavi imefanikiwa kumkamata jangili Jonathan Charles
mkazi wa Ulwila akiwa na silaha moja ya kivita aina ya smg ikiwa na risasi
30 ndani yake
Akizungumza na waandishi wa habari kaimu kamanda wa polisi
mkoa wa Katavi Joseph Myovela amesema poaresheni hiyo ilifanyika katika eneo la
Ilumbi ndani ya hifadhi ya taifa wilaya ya Mpanda kwa lengo la kuwasaka
wawindaji haramu wenye silaha za kivita nab ado jeshi hilo linawasaka watu watatu
Amesema bunduki hiyo iliyokamatwa ni namba M22/13350 ambapo
kukamatwa kwa mtuhumiwa huo kumetokana na mtego uliowekwa ambapo baada ya
kuzingirwa majangili hao walianza kufyatua risasi hali iliyopelekea kukamatwa
kwa mtuhumiwa mmoja