RC MAHIZA
Mkuu wa mkoa wa Pwani Mh. Mwantumu Mahiza amesema mkoa wake
utawachukulia hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwakamata na kuwafikisha
mahakamani watu wote wanaowahamasisha wakazi wa mkoa huo kutoshiriki katika sensa ya watu na makazi
itakayofanyika Agosti 26, mwaka huu
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mahiza
amesema imefikia hatua hiyo kutokana na kuwepo kwa baadhi ya makundi ya watu
ambao wanahamasisha wananchi kususia kushiriki katika zoezi la sensa kwa
kisingizio cha dini na kisingizio cha korosho kukosa soko
Katika taarifa yake aliyoitoa kwa waandishi wa habari
amesema endapo itatokea mtu ama kikundi cha watua ambacho kitazuia familia
yeyote isitoe taarifa wakati wa sensa ya watu na makazi atakuwa amefanya kosa
la jinai hivyo ni lazima achukuliwe hatua za kisheria

