
FFU
wakiwa wameuzuia msafara wa viongozi wa Chadema Taifa eneo la
Miyomboni mjini Iringa jioni hii ,msafara huo ulikuwa ukitokea
Morogoro kuja Iringa
Msafara
wa Chadema ukiwa umepigwa Stop eneo la Miyomboni jioni hii

Jeshi
la polisi mkoani Iringa limeuzuia kwa muda msafara wa viongozi wa
kitaifa wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) ambao
walikuwa wakiingia mjini Iringa wakitokea mkoani Morogoro.Askari
polisi hao wakiongozwa na askari wa FFU zaidi ya 100 waliuzuia
msafara huo eneo la Zebra katika barabara kuu ya Iringa - Dodoma baada
ya jeshi hilo awali kuzuia maandamano ya Chadema na vyama vyote kwa
maelekezo ya msajili wa vyama vya siasa.Hata hivyo kutokana
na umati mkubwa wa wananchi mkufika eneo hilo viongozi wa Chadema na
polisi waliweza kukubaliana msafara huo kuendelea na safari yake
kuelekea nyumbani kwa mbunge Msigwa eneo la Kihesa .Katika
tukio hilo jeshi la polisi halijaweza kutumia mabomu wala nguvu
zaidi katika kuwatawanya wananchi kama ilivyo kuwa mkoani Morogoro
jana.
HABARI: www.francisgodwin.blogspot.com
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi