MAMA mmoja
akiwa na watoto wake saba pamoja na
wananchi wengine wawili wakazi wa kijiji
cha Turugeti Kata ya Bumera Wilayani Tarime Mkoani Mara wameandamana hadi
ofisi ya Mkuu Waliya ya Tarime
wakidai kubomolewa nyumba zao jana
na mtu mmoja aitwae Manyengo
Lautent baada ya kudai kuwa eneo
wanaloishi watu hao si lao bali walivamia.
Wakieleza
malalamiko yao mbele ya katibu Tawala wa
Wilaya ya Tarime Hernest Kabohola walisema kuwa mnamo agost 28 majira ya
saa 6
mchana Manyengo Laurent mkazi wa mjini
Tarime alifika kijijini hapo akiwa ameongozana na kundi la watu zaidi ya
30 na
polisi wa Kituo cha Turugeti na kisha wakaanza kubomoa nyumba zao kwa
kile
walichodai kuwa watu hao wamevamia na
kuishi kwenye eneo la Manyengo Laurent.
“ Jana
majira ya saa 6 Manyengo alikuja na
kundi la watu akachukuwa polisi wa Turugeti
wamebomoa nyumba zetu wanasema tuhame eneo hili tumehamia wakati wa
oparesheni
vijiji leo hii naambiwa nihame niende
wapi na mi ni mzee! Serikali itusaidie sheria itumike ipasavyo”alisema
Gitera
Marwa.
Mwita Mkori
alisema kuwa anashangaa kuona nyumba yake inabomolewa kwani
hajawahi kushitakiwa mahali popote
kuhusu eneo hilo lakini nyumba yake
imebomolewa bila taratibu za kisheria
kufuatwa licha yakuwa eneo hilo alilimiliki tangu wakati wa oparesheni
vijiji
mwaka 1974.
Rhobi Ryoba
alisema kuwa kitendo cha nyumba yake
kubomolewa na kutakiwa kuachia eneo limeathiri familia yake kwakuwa hawana mahali pa kuishi yeye na
familia yake ambapo kwa sasa wanaifadhiwa na
majirani.
“Nitaenda
wapi nawatoto 7 na nina ujauzito mme wangu yuko jela alihukumiwa kifungo
cha
mwaka mmoja na mahakama ya Mwanzo Tarime
kutokana na tatizo hilihili la Manyengo Laurent, Mahakama
ikaamuru
nyumba yangu ibomolewe kuwa eneo si letu
leo wamekuja wamebomoa japo eneo hilo tumeishi tangu wakati wa
oparesheni
vijiji wakati huo manyengo akiishi Dar es Salaamu baadae
akahamia mjini Tarime na sasa kaja kijijini anadai eneo ni la babu yake kashitaki mme
wangu na kisha amebomoa Naomba msaanda wa Serikali utatue tatizo
hili”alisema
Rhobi
Katibu
tawala wa Wilaya ya Tarime Hernest Kabohola aliwataka wananchi hao
kurejea katika uongozi wa Serikali ya kijiji ili
tatizo lao lishughulikiwe kwakuwa wao
ndio wanatambua eneo kwa uhalisia.
Mtendaji wa
kijiji cha Turugeti Matiko Chegere
alisema kuwa wananchi hao ndio wamiliki
halali wa eneo kwani wameishi kwa muda mlefu tangu wakati wa oparesheni
vijiji
na kuwa anasikitika wananchi wengine kubomolewa nyumba kwakuwa
hawajawahi
kushitakiwa mahali popote na wala ofisi yake na uongozi wa serikali ya
kijiji
haukupewa taarifa na Manyengo Laurent kuhusu
ubomoaji wa nyumba,nakwamba eneo si la Manyengo Laurent.
Kamanda wa
polisi Tarime/Rorya alipohojiwa kama ana taarifa juu
ya polisi wake kuhusika katika zoezi la
ubomoaji nyumba alisema ofisi yake haina taarifa hiyo na hivyo kuahidi
kufatilia swala hilo kwa ukaribu.