Jeshi
la polisi mkoa wa Iringa limetoa tahadhari kwa wananchi kuwa makani
na fedha wanazolipwa ili kuepuka kubambikizwa noti bandia ambazo
tayari jeshi hilo limekamata zaidi ya bandia zenye thamani ya zaidi
ya shilingi 700,000.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda amesema leo kuwa noti hizo zimekamatwa na askari polisi baada ya kupata taarifa kutoka kwa wananchi wasamaria wema.
Kamuhanda alisema kuwa hadi sasa jeshi hilo la polisi linawasaka wahusika wa mtandao huo wa kusambaza noti bandia katika mkoa wa Iringa ili kuchukuliwa hatua za kisheria.
Alisema kuwa fedha hizo ambazo zimekamatwa katika maeneo tofauti tofauti zina namba ambazo zinafanana na hivyo kuwataka wafanyabiashara na wakulima kuwa makini na watu wanaofika kununua mazao yao

HABARI KWA HISANI YA www.francisgodwin.blogspot.com.