Chadema na polisi walijikuta katika
mvutano mkali na kuzungushana huku na kule jana baada ya viongozi wa Chadema mkoa
wa Iringa kushikilia msimamo wao wa kuwepo
kwa mkutano huo katika viwanja vya mwembetogwa pamoja na
jeshi la polisi kuzuia
mkutano huo.
Mwandishi wa
habari hizi alishuhudia mvutano huo mkali baada
ya askari wa kikosi cha
kutuliza ghasia (FFU) wakiongozwa na kamanda wake
Mnunka wakitanda eneo la uwanja wa
mkutano eneo la Mwembetogwa huku viongozi wa Chadema wakizunguka huku na kule mjini
Iringa kushinikiza mkutano huo.
Mbali ya askari hao
kumwagwa eneo la uwanja wa
Mwembetogwa na hata kuzuia wafanyabiashara ndogo ndogo eneo hilo kuondoka
,bado idadi kubwa ya askari walionekana wakizunguka maeneo mbali mbali ya mji
wa Iringa huku baadhi yao
wakiwa wametanda nje ya ofisi ya Chadema wilaya ya Iringa mjini eneo la
Mshindo kama njia ya kuzuia viongozi hao kutoka kwa maandamano eneo
hilo.
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Chiku Abwao (Chadema)
ambaye pia ni mjumbe
kamati kuu Taifa alisema kuwa kutokana na
mvutano huo wa jeshi
la polisi na Chadema wameamua kutoufanya
mkutano huo leo
Abwao alisema kuwa kutokana na hoja hiyo ya polisi
ya kuwa kwa
sasa ni zoezi la sense
ya watu na makazi wamelazimika kutii
agizo hilo na hivyo kuamua kusogeza mbele mkutano huo.
Hata hivyo alisema baada ya jeshi la polisi kutangaza
kusitisha mkutano huo kwa
upande wake alilazimika kutangaza katika vyombo mbali mbali vya habari zikiwemo
radio za mkoa wa Iringa ili kusitisha mkutano huo japo
tayari kulikuwepo na maandalizi makubwa ya mkutano huo.
Hata hivyo Abwao aliwaomba radhi wananchi wa jimbo
la Iringa mjini ambao walikuwa tayari kushiriki mkutano huo na kuwaomba wajiandae kwa wakati mwingine ambao chama hicho kitatangaza mkutano huo.
"Chadema tumetumia busara kuepusha shari zaidi kati ya polisi na
chama pia kuepusha wananchi kumwaga damu"
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda alieleza sababu za kuzuia
mkutano huo kuwa ni baada ya kupokea agizo kutoka kwa msajili wa vyama vya siasa nchini hasa baada ya
tukio la Morogoro jana
Hivyo alisema kwa sasa wakati zoezi la sense
linaendelea chama chochote
cha siasa hakitaruhusiwa kufanya
mkutano wa hadhara hadi
hapo zoezi hilo la Sensa litakapokamilika.
chanzo www.francisgodwin.blogspot.com