WAKULIMA wa zao la kahawa katika jimbo
la Vunjo
wamelalamikia urasimu unaofanywa na taasisi ya utafiti wa kahawa nchini
(tacri)kwa kutofikisha huduma zao maeneo mengi ya vijijini ambapo ndipo
wakulima wengi wanakopatikana.
Wakulima hao walitoa kilio chao katika
mikutano
ya hadhara mbele ya mbunge wa jimbo hilo Agustine Mrema na kudai kuwa
taaisi
hiyo inaonekana kuwanufaisha watu wachache na sio wakulima kama uhalisia
wa
taasisi hiyo.
Mwenyekiti wa chama cha msingi cha
Mrimbo
Uuwo Livingstone Shao alisema kuwa taasisi ya utafiti wa kahawa nchini
(TACRI)imekuwa ikiwafanya wakulima walio wengi kushindwa kupata pembejeo
au
elimu juu ya utunzwaji wa zao hilo.
‘Mh mbunge TACRI tumekuwa tukiisikia
tu ila
hatujawahi kunufaika na taasisi hii sasa sijui kama inashia mjini kama
kutakuwa
na wakulima wa zao hili kweli”alisema mwenyekiti huyo
Mbali na taasisi hiyo kutofika maeneo
ya
vijijini bado walilalamikia kutopatikana kwa miche ya kahawa ambapo hata
ikiopatikana huuzwa kwa bei ghali jambo ambalo mkulima wa kawaida
anashindwa
kumudu.
Mbunge wa jimbo hilo Agustine Mrema
aliwataka
wakulima hao kuweza kuandika malalamiko yao ili aweze kuyashughulikia na
kufikisha katika ngazi husika ili yaweze kutatuliwa na kupatikana kwa
suluhu ya
kudumu.
Mrema alifanya ziara katika kata ya
Mwika kaskazini na kuweza kuongea na wananchi katika mikutano ya hadhara
katika
vijiji vya Lole ,na Mrimbo uuwo.
