KATIBU Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod
Slaa, amefukuzwa katika nyumba ya kulala wageni iliyoko ndani ya Chuo
cha Ufundi Stadi (Veta), cha Mikumi wilayani Kilosa, Mkoa wa
Morogoro kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni sababu za kisiasa.
Tukio hilo
lililoambatana na kuzimwa kwa umeme katika mji mdogo wa Mikumi na
vitongoji vyake kwa siku nzima, limetafsiriwa na Dk Slaa kuwa ni hila
zinazofanywa na CCM kuhujumu operesheni ya Chadema ya Vuguvugu la
Mabadiliko (M4C) inayoendelea katika wilaya mbalimbali mkoani humo.
Dk Slaa aliwasili
chuoni hapo majira ya saa 8.00 mchana akitokea wilayani Ulanga katika
Operesheni M4C ikiwa ni mwendelezo wa Operesheni Sangara iliyofanyika
katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Baada ya kuwasili
katika hoteli ya chuo hicho, Dk Slaa alipokewa na wahudumu wa hoteli
hiyo na kukabidhiwa funguo ya chumba namba tano ambacho Mkurugenzi wa
Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare, alikiomba kwa ajili
yake.
Muda mfupi baada ya
kuchukua funguo hizo, akatokea meneja wa hoteli hiyo ambaye jina lake
halikufahamika mara moja na kumweleza Dk Slaa kuwa sehemu hiyo
imeshawekewa ‘booking’ hivyo Dk Slaa aondoke.
Tukio hilo lilimfanya
Dk Slaa ahoji mantiki ya hatua hiyo hasa, baada ya mhudumu wa hoteli
hiyo kumkubali na kukabidhi funguo kwake na meneja huyo kumnyang'anya
funguo hiyo.
Funguo
ya chumba alichotakiwa afikie Dk Slaa alikabidhiwa Mkurugenzi wa Ulinzi
na Usalama wa Chadema, Rwakatare baada ya kukiomba chumba hicho siku
kadhaa nyuma.
Hata
hivyo, meneja huyo alisisitiza Dk Slaa kuondoka kwa kuwa yeye hakuwa na
taarifa na ujio wake.
Kufuatia
tukio hilo Dk Slaa aliondoka na kuelekea katika eneo la mkutano wa
hadhara ambako pia umeme ulizimwa ghafla hivyo, kuongozea hisia kwa Dk
Slaa kuwa alikuwa anahujumiwa kwa kuwa hakukuwa na ratiba ya mgawo wa
umeme siku hiyo.
Akizungumza katika mkutano wake huo, Dk
Slaa alikituhumu CCM kuwa ndiyo kilichoandaa mpango huo kwa lengo la
kuhujumu kampeni zake za kumkomboa Mtanzania.
Hata hivyo, Katibu wa
Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alipuuza madai hayo ya Dk Slaa
akisema, "Namshauri aache siasa kwa kuwa zimeanza kumshinda,"
Nape alisema Dk Slaa hawezi kueleweka
kukihusisha CCM na kufukuzwa kwake hotelini kwani hoteli hiyo ya Veta,
siyo mali ya chama hicho tawala.
"Dk Slaa amezeeka. Aache siasa awaachie
vijana. Yeye afukuzwe huko halafu aseme CCM tunamhujumu! Namshauri
apumzike siasa awaachie vijana waendeleze gurudumu," alisema Nape.
Meneja wa Tanesco, Mkoa wa Morogoro,
Deogratius Ndamugaba, akijibu shutuma za kukatika kwa umeme katika mji
huo alisema kuwa kukatika huko kulitokana na hitilafu za kawaida na siyo
hujuma au msukumo wa kisiasa.
“Kukatika
kwa umeme Mikumi si kwa sababu ya Chadema ila ni feeder ya Mikumi iko
nje tangu saa 12.45 jioni, nguzo imeanguka na inapaswa kubadilishwa na
sehemu yenyewe ni porini, kuna giza na chui,” alisema meneja huyo.
Slaa
amvaa Nape
Katika hatua nyingine, Chadema kimemtaka Mwenyekiti wa
CCM, Rais Jakaya Kikwete kutoa elimu kwa viongozi wa chama hicho tawala kuzungumza kwa busara mbele ya wananchi kwani kinyume chake wanamletea sifa mbaya.
Akizungumza katika mikutano ya hadhara ya chama hicho katika vijiji mbalimbali vya Wilaya ya Ulanga, mkoani Morogoro, Dk Slaa alisema kuwa ni kawaida ya mtu mwenye tabia mbaya kama vile mwizi kujishtukia na kufikiria kuwa hata wenzake ni wezi.
Alisema kuwa ni aibu kwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete kuachia viongozi walio chini yake ndani ya chama hicho kutoa matamko yanayoivua nguo Serikali kuwa haiko makini na inazidi kukupoteza dira na mwelekeo wake.
“Nataka nimalizie na suala moja ambalo limetokea leo mchana. Kuna tamko moja limetolewa na kijana mmoja wa CCM anaitwa Nape, sasa kwa sababu ni kama kinda la njiwa kwangu, sitamjibu yeye. Alichokisema kwa watu wanaojua, tunamshangaa Kikwete kwa kuachia mambo ya chama chao na Serikali yake kwa jumla.

Chanzo
- Mwananchi
.jpg)