SHERIAYA
TAKWIMU, SURA 351(THE STATTISTICS ACR, CAP.351
1.0
Utangulizi
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ni Wakala
wa Serikali yenye mamlaka ya kisheria ya kutoa takwimu rasmi nchini.
2.0 Mjukumu
ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu yameainishwa katika Sheria yaTakwimu, 2002
(Na.1, 2002). Miongoni mwa majukumu hayo ni
kuendelesha zoezi la Sensa ya Watu na Makazi katika
Jamhuri ya Mungano wa Tanzania(To conduct population and Housing
Census in the United Republic). Kifungu cha 5(1)(a) cha Sheria ya
Takwimu, 2002.
Aidha , Sheria hiyo inaelekeza kuwa katika kutekeleza majukumu ya
kitakwimu ambayo yanaihusisha Tanzania na Zanzibar, NBS itashirikiana
na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya, Zanzibar (Office
oa Chief Gornment Statatician-OCGS). Kifungu cha 5(2) cha Sheria ya
Takwimu, 2002.
3.0 Kiapo cha kutunza siri(Oath
of secrecy)
Shughuli za NBS ni za kipekee kwa kuwa zinahusu
ukusanywaji wa taarifa zinazohusu maisha ya mtu binafsi. Kwa mantiki
hiyo, taarifa hizo zinahitaji usiri mkubwa. Katika kudhihirisha jambo
hilo, sheria ya Takwimu inaeleza kuwa mtu atakaye husika katika zoezi la
ukusanyji wa takwimu ikiwa ni pamoja na takwimu
za Sensa ya Watu na Makazi, atalazimika kuapishwa (kiapo cha
kutunza siri) mbele ya Kamishna wa viapo (Commissioner for Oaths)
kabla ya kuanza kazi husika. Kifungu cha 11(2) cha Sheria ya
Takwimu, 2002.
4.0 Maofisa
walioidhinishwa (authorized Officersa
Katika
kutekeleza majukumu yake, Mkurungenzi Mkuu
amepewa mamlaka ya kuwaidhinisha watu wengine kwa lengo kukusanya
taarifa maalum za kitakwimu kulingana na mahitaji.
Kifungu cha Sheria ya Takwimu,
2002.
5.0
Amri ya Rais kuhusu
kufanyika kwa Sensa ya Watu na Makazi
Sensa ya Watu na Makazi ni shughuli ya kitaifa ambayo
katika utekelezaji inahusisha maelekezo ya Rais wa Nchi. Sheria ya
Takwimu inaeleza kuwa kabla zoezi la Sensa ya Watu na Makazi
halijafanyika, Rais anatakiwa kutoa Amri (Presidential Order) ya
kufanyika kwa Sensa. Amri hiyo inatakiwa kueleza:-
a) Tarehe ya kufanyika kwa Sensa;
b) Taarifa zitakazokusanywa katika Sensa;
c) Namna Sensa itakavyofanyika;
d) Muda na mahali Sensa itakapofanyika; na
e) Wahusika katika kukusanya taarifa za Sensa
Kifungu cha 14 cha Sheria ya Takwimu, 2002
6.0 Makosa ya Jinai na Adhabu zake
Sheria ya Takwimu inaainisha
vitendo ambavyo ni makosa ya jinai na pia Sheria hiyo inaweka wazi
adhabu zinazoweza kutolewa kwa yeyote ambaye atakuwa ametenda makosa
hayo.
Kifungu cha 27 cha Sheria ya Takwimu, 2002 kinabainisha
makundi ya aina tatu ya
watu wanaoweza kushtakiwa kutokana na viten do ambavyo ni makosa kwa
mujibu wa Sheria hiyo.
6.1
Waajiriwa wa NBS/
Wadadisi/ Wasimamizi(Authorized Officer)
a. Kutumia taarifa za kitakwimu kwa manufaa binafsi
(use of information for personal gain);
b. Kutoa taarifa za kitakwimu bila kibali
(publishing any information without authority);
c. Kutoroka/kutelekeza kazi uliyopangiwa kuifanya
(desertion);
d. Kudai taarifa tofauti na
zilizoruhusiwa kukusanywa (obtaining information not authorized to
obtain); na
e. Kuomba malipo/ujira(asking
payment or reward).
Vitendo hivyo vyote ujumla
ni makosa ya jinai na mhusika akipatikana na
hatia atastahili adhabu ya kifungo
cha miezi 12 au kulipa faini ya shilingi milioni moja au vyote viwili. Kifungu cha 27(1) a-e) cha Sheria ya Takwimu, 2002.
6.2
Kutoa taarifa
zilizopatikana isivyo halali (Mtu yeyote)
Sheria hii inabainisha kuwa ni kosa kwa
mtu yeyote kukutwa au kutoa taarifa za kitakwimu zilizopatikana
kwa kukika vifungu vya Sheria ya Takwimu. Adhabu
kwa makosa ya kundi hili ni kifungo
cha miezi 18 au faini ya shilingi milioni moja na laki tano au vyote viwili. Kifungu
cha 27(2) cha Sheria ya Takwimu, 2002
6.3
Kutotoa ushirikiano
katika zoezi la kitakwimu (Respondent/ Mtu yeyote)
Sheria hii pia inaainisha makosa yanayowezakufanywa na
mtu yeyote au Respondent wakati wa zoezi la kitakwimu (wakati wa kukusanya takwimu).
Makosa hayo ni:
a. Kumzuia Authorized Officer
(Msimamizi/Mdadisi/Karani wa Sensa kutekeleza majukumu yake
b. Kukataa /kuacha kwa
makusudi:
i. Kujaza fomu au nyaraka
yoyote iliyokabidhiwa kwake kwa lengo maalum;
ii. Kujibu maswali aliyoulizwa;
c. Kutoa taarifa za uongo
d. Kuharibu au
nyaraka yoyote
e. Kujifanya Authorized
Officer kwa lengo la kujipatia taarifa ambazo hastahili kuzipata;
f. Kukataa kutoa nyaraka
zozote zinazohitajika katika shughli za kitakwimu;
g. Kukiuka kifungu chochote
cha Sheria hii.
Sheria inaeleza kuwa adhabu kwa kosa lolote kati
ya hayo ni kifungo cha miezi 6 au faini ya shilingi laki sita. Kifungu cha 27(3) cha Sheria ya Takwimu, 2002.
7.0
Hitimisho
Sheria ya Takwimu, 2002 imeainisha majukumu ya NBS na
kutamka wazi aina za makosa na adhabu zake.
Kwa mantiki hiyo ni kjukumu la kila mmoja kutimiza
wajibu wake na kutoa ushirikiano unaostahili katika zoezi la Sensa ya
Watu ma Makazi ya Mwaka 2012.
Kwa kufanya hivyo, kila mdau
atakuwa ameisaidia Serikali kupata taarifa sahihi kwa ajili ya mipango
ya maendeleo ya nchi.
SENSA KWA MAENDELEO: JIANDAE
KUHESABIWA

