HAI
MKUU wa wilaya ya Hai bw.Novatus Makunga amewaagiza viongozi wa
vijiji na kata kusimamia miradi ya maendeleo sanjari na kudai stakabadhi zinazoonyesha kiasi cha fedha zinazotumika katika miradi inayoanza kutekelezwa katika maeneo yao.
Makunga ametoa agizo hilo baada ya kukagua ujenzi wa barabara ya
kilometa sita na nusu ya vijiji vya kata ya machame Mashariki, inayounganisha njia panda ya Makoa na vijiji vya Nkuu Sinde, Foo na Nronga inayojengwa na serikali kwa Sh.Milioni 20 kwa kiwango cha Moramu.
Amewataka viongozi wa vijiji kusimamia kila mradi unaotambulishwa
katika vijiji vyao kwa kuwa na nyaraka zinazoonyesha aina ya mradi na
idadi ya vifaa vitakavyotumika ili kudhibiti vitendo vya uchakachuaji
wa miradi hiyo.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa vijiji hivyo bw.Isaya Mlengeni
ameeleza kuwa,kabla ya ujenzi wa barabara hiyo,walikuwa wanatembea
umbali mrefu kwa miguu kutokana na ubovu wa barabara hiyo.
Amesema kutokana na ubovu huo,wananchi hao awali walikuwa wakitegemea usafiri wa pikipiki ambapo nauli yake ilikuwa juu na kuishukuru serikali kwa kuwatengenezea barabara hiyo na kusema kuwa kukamilika kwa barabara hiyo ni mkombozi kwa wananchi hao.