MAKETE
Chama
cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) wilayani Makete kimewataka wananchi wote
kushiriki kikamilifu katika sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika
usiku wa kuamkia Agosti 26 mwaka huu
Akizungumza
na mwandishi wetu Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Makete Shaaban Mkakanze
amesema suala la sensa halina itikadi za vyama bali ni kwa maendeleo ya taifa
hivyo wananchi wajitikeze kuhesabiwa
“Sisi
kama CHADEMA hatuna ubishi wala hatukatazi watu kushiriki katika sensa,
tunahimiza watu wote wajitokeze kushiriki sensa, na hata sisi kwenye mikutano
yetu ya hadhara hapa Makete tunawahimiza wananchi wote wajitokeze kwa wingi
katika sensa” alisema
Katika
hatua nyingine Mwenyekiti huyo amewashukuru wananchi waliotoa michango yao kufanikisha
mikutano waliyoifanya katika tarafa ya Ikuwo, na kuwaomba wananchi wenye
mapenzi mema na chama hicho kuendelea kutoa michango yao ikiwa ni pamoja na
kukisaidia kushiriki wa mgombea wa chama hicho katika uchaguzi wa diwani wa
kata ya Luvumbu wilayani hapo
Amesema michango
ya wananchi hao itatangazwa kwenye vyombo vya habari lakini kama yupo aliyetoa
michango na hataki itangazwe wao kama CHADEMA watazingatia hilo  , hivyo kusema chama hicho hakina ubaya
na mtu bali kinaipa changamoto serikali iliyopo madarakani ili ijisahihishe
kutokana na changamoto zinazoikabili
