Kikosi cha
timu ya Yanga kikiwa katika picha ya pamoja kwenye uwanja wa Taifa kabla
ya kuingia uwanjani
Kikosi
cha timu ya Africa Lyon kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mpambano
huo kuanza.
Katika mchezo wa Yanga na Africana Lyon, Yanga imeibuka na ushindi
wa Mabao 4-0. Bao la kwanza la Yanga, limefungwa na kipa wa African
Lyon, Juma Abdul, aliyejifunga katika dakika 8, kipindi cha kwanza, bao
la pili limefungwa na Haruna Niyonzima kwa mkwaju wa penati, dakika ya
54, baada ya beki wa Lyon Semi Kessy, kumchezea rafu, Msuva katika eneo
la hatari. Goli la tatu limefungwa na Simon Msuva, katika dakika ya 72,
kufuatia pasi safi ya Frank Dumayo na bao la nne limefungwa na Jerry
Tegete katika dakika ya 90+2, baada ya pasi safi ya Idrisa Rashid.

