Wafanyabiashara Kariakoo wagoma kumfuata Waziri Mkuu Dodoma

Hadi saa 4.10 asubuhi hali ni tofauti na siku zote katika soko maarufu la Kariakoo ambapo maduka yamefungwa, hakuna msongamano wa watu katika mitaa yake wala kelele za wamachinga wakipishana kuuza bidhaa zao.


Huo ni utekelezaji wa msimamo wa wafanyabiashara wa Kariakaoo ambapo wameazimia kuanzia leo Jumatatu Mei 15, 2023 wanafunga maduka yao kwa ajili ya kushinikiza Serikali kuingilia kati kuanzishwa kwa sheria na tozo wanazodai zinazowakandamiza ikiwemo zile zinazotaka stoo walizonazo kusajiliwa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa wafanyabiashara katika soko hilo, Martin Mbwana amejitoa katika kile kinachoendelea Kariakoo kwa kusema yeye ni mjumbe wao tu hivyo watakachoamua ndiyo watafanya.

"Mimi ni messenger (mjumbe) tu mtakachoamua nyie ndio kile nitakachokifuata," amesema Mwenyekiti huyo katika kikao na wafanyabiashara hao.

Jambo hilo liliwafanya wafanyabiashara eneo hilo kushangilia kwa sauti huku wakisema mwisho wa kuonewa umefika.

Kwa upande wake Mfanyabiashara, Justin Massawe amesema "Sisi tumesema hatufungui na tuko tayari kwenda shambani tukalime mpaka kero zetu zitakaposikilizwa," amesema.

Awali majira ya saa 2 asubuhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla alifikia katika soko hilo na kuzungumza na wafanyabiashara hao huku akiwataka wajumbe kusafiri nae kwenda Dodoma kwa ajili ya kikao na Waziri Mkuu jambo ambalo baadae katika kikao cha wafanyabiashara peke yao lilikataliwa.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo