Spika Tulia ajibu mapigo wanaolitaka jimbo la Mbeya Mjini

Hatimaye Spika wa Bunge, Tulia Ackson amevunja ukimya kwa kusema wanaotaka kugombea ubunge Mbeya Mjini wapime kina cha maji kama kinawatosha waingie kwenye kinya’ng’anyiro.


Spika Tulia ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini ametoa kauli hiyo leo Mei 4, 2023 Alhamisi wakati wa mahojiano na kituo cha runinga cha Wasafi TV hapa nchini akiwa katika makazi yake Jijini Dodoma.

Katika mahojiano hayo Dk Tulia ameeleza sababu za kutaka jimbo hilo kugawanywa akisema suala hilo halihusu Mbeya Mjini pekee bali katika majimbo mbalimbali makubwa na hatua hiyo itasaidia kusogeza huduma karibu.

“Ubunge wangu haijalishi jimbo limegawanya au halijagawanywa, mimi ndio Mbunge kama nilimtoa mtu (Sugu) katika kata 36, hataweza kunitoa kata zikiwaa chache kweli? Mbona itakuwa mtihani, zikibaki kata 36 nitawafyeka.

“Nisingeshangaa kujadiliwa na wao, tena napenda sana wao wameanzisha huo mjadala nimefurahi na wanaposema watanifuata, nataka wajipime kama wanaona kina cha maji cha kinawatosha waje, kama niliwatoa na kata 36 wataniweza wapi na kata chache? amehoji Dk Tulia.

Kauli hiyo imekuja baada ya jana Jumatano, Bunge kutaarifikiwa kuwa kiongozi huyo ni miongoni wa wabunge waliowasilisha maombi ya kugawa majimbo yao ili kuwa mawili kutokana na ukubwa na wingi wa watu na hivyo kurahisisha shughuli za maendeleo.

Chanzo: 
mwanachidigital


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo