Auawa na tembo akitaka kupiga naye picha Tabora

Mwanaume Aliyefahamika kwa jina la John Siame (46) mkazi wa kijiji cha Ifuta kata ya Ukondamoyo wilaya ya Urambo mkoani Tabora ameuawa kwa kukanyagwa na tembo alipokwenda na wenzake kuwafukuza na kutaka kupiga picha na tembo wawili waliokuwa wamezama kwenye matope.


Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha ifuta Mussa Kanyele amesema tembo wawili walizama kwenye tope wakati wananchi walipojaribu kulifukuza kundi la tembo waliovamia kijiji hicho

Amesema baada ya kunasa kwenye tope wananchi kadhaa waliwasogelea na kutaka kupiga nao picha jambo lililompandisha tembo mmoja ghadhabu na kuwakimbiza wananchi hao kisha kumkanyaga na kumuua mwananchi huyo.

kwa upande wale afisa mtendaji wa kijiji cha Tumaini Jeofrey Magambo amesema wakati wanasubiri msaada wa maafisa wanyamapori walifanikisha kuwatoa tembo kwenye eneo lenye watu wengi na kuwasogeza mbali kidogo ili kuhakikisha usalama wa wananchi licha ya tembo hao kuendelea kusalia eneo la kijiji.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo