LATRA yaruhusu mabasi kufanya safari usiku

Mamlaka Udhibiti Usafi ri Ardhini (LATRA) imeruhusu mabasi ya mikoani yaanze safari saa tisa usiku. 


Latra imeagiza wamiliki wa mabasi wanaopenda kuanza safari muda huo wafike katika ofisi za mamlaka hiyo kuomba leseni na masharti ni lazima madereva wasajiliwe ili kuwa na taarifa zao.


Katibu Mkuu wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (Taboa), Priscus Joseph amesema hayo Dar es Salaam akiwa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Latra, Salum Pazzy.

Pazzy aliwaeleza waandishi wa habari kuwa Latra inafanya kazi kwa kushirikisha na wadau wakiwamo Taboa na hawana mvutano kuhusu muda wa kuanza safari za mabasi kwenda mikoani.

“Tunafanya kazi kwa kushirikiana, suala la kubadilisha ratiba za mabasi awali muda ulikuwa ni mabasi yote lazima yaanze safari saa 12 asubuhi si zaidi ya hapo, lakini baadaye tuliruhusu ratiba zianze saa 11 asubuhi,” alisema.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo