Wanafunzi wawili wafariki wakisaidia kujenga darasa

Wanafunzi wawili wa shule ya msingi Shashui iliyopo Kata ya Soni, wilayani Lushoto, Mkoani Tanga, wamefariki baada ya kuangukiwa na ukuta wa darasa, huku ikidaiwa kuwa waliagizwa na mwalimu kumsaidia fundi kujenga darasa hilo , baada ya kuezuliwa paa.


Akizungumza na wananchi alipofika kwenye tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Kalist Lazaro, amesema tayari Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, fundi na walimu wengine watatu wamekamatwa kwa ajili ya mahojiano juu ya tukio hilo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo