Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ameguswa na kifo cha aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya nje, Bernard Membe na kutoa pole kwa familia.
Kupitia mitandao yake ya kijamii, Rais Samia ameandika ujumbe wake huo kuonesha jinsi alivyopokea taarifa hizo za kifo.
"Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Ndugu Bernard Membe. Kwa zaidi ya miaka 40, Ndugu Membe alikuwa mtumishi mahiri wa umma, mwanadiplomasia, Mbunge na Waziri aliyeitumikia nchi yetu kwa weledi. Pole kwa familia, ndugu, jamaa & marafiki. Mungu amweke mahali pema. Amina."
Membe (70) amefariki dunia leo Ijumaa, Mei 12, 2023 katika Hospitali ya Kairuki mkoani Dar es Salaam.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa Membe alipata changamoto ya kifua na kupelekwa alfajiri ya leo Hospitalini hapo na baadaye kufariki.
Naye Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Camilius Membe kilichotokea mapema leo katika Hospitali ya Kairuki Jijini Dar es salaam.
Mbowe amesema “Membe aliitumikia Nchi yetu katika ngazi mbalimbali na alikuwa hazina muhimu kwa Taifa.
“Raha ya milele umpe ee bwana, na mwanga wa milele umuangazie, apimzike kwa amani”Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya Benard Membe aliyefariki asubuhi ya leo akieleza jinsi alivyomfahamu na kufanya kazi na mwanasiasa huyo.
Membe ambaye alikuwa mwanachama wa CCM alijiunga ACT Wazalendo Julai 15 mwaka 2020 kisha kurejea CCM Mei 29 mwaka 2022.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter Zitto ameandika, “Hakuna maneno yanayoweza kueleza mstuko mkubwa nilioupata kufuatia Taarifa ya msiba huu, zaidi ya kumshukuru Mungu muumba kwa Maisha ya Mzee wetu Bernard Kamilius Membe ambaye amefariki Dunia Leo asubuhi. Mwanasiasa mahiri, mwanadiplomasia maarufu na mwakilishi wa Wananchi.
“ Kwa niaba yangu Binafsi na kwa niaba ya Wanachama wa Chama cha ACT Wazalendo ambaye BM aliwahi kuwa mwanachama wake natoa pole kwa familia, ndugu, Jamaa, marafiki na Wananchi wote wa Jimbo la Mtama Nnauye Nape na Mkoa wa Lindi Isiha kamchinji kufuatia msiba huu mkubwa. Tupo pamoja katika kipindi hiki cha majonzi,”ameandika Zitto.