Muumini aliyeokolewa baada ya kufunga, agoma kula chakula

Mnamo Jumapili, Aprili 23, makachero kutoka Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) wamefukua miili 18 zaidi katika Msitu wa Shakahola, Kilifi, nchini Kenya inayoaminika kuwa ya wafuasi wa mchungaji tata Paul Mackenzie.


Miili sita ilipatikana kwa mara ya kwanza kwenye makaburi matatu yenye kina kirefu. Saa chache baadaye, miili 12 zaidi ilipatikana katika makaburi saba, na hivyo kuongeza idadi ya mateka wa mchungaji huo kufikia 39.


Muumini wa Mackenzie akataa chakula Wakati wa zoezi hilo, wapelelezi walimuokoa mwanamke mmoja ambaye anasemekana alikuwa katika hali mbaya kiafya.


Hata hivyo, mwanamke huyo aliwashangaza wapelelezi na maafisa wa Shirika la Msalaba Mwekundu akionyesha ishara kwamba hataki kutibiwa. Wakati maafisa wa afya walipojaribu kumpa maji yaliyochanganywa na sukari ili kumpa nguvu, mwanamke huyo alikaza mdomo wake kwa nguvu. Mwanamke huyo aliyekuwa hoi, alionyesha ishara kwamba hataki kutibiwa bali aachwe afe.


Pasta Mackenzie akataa chakula gerezani Awali, iliripotiwa kwamba mtumishi wa Bwana mwenye utata Paul Mackenzie kutoka kanisa la Good News International amekataa kula chakula gerezani. Mackenzie anazuiliwa baada ya kuibuka kuwa aliwashawishi washirika wake kufunga kula hadi kufariki dunia. Ripoti ya polisi inasema Mackenzie amekuwa akikataa kula wala kunywa chochote tangu alipokamatwa kuhusiana na vifo vya washirika wake.


Makachero walisema kwa wakati mmoja walitaka kumpa kikombe cha maji lakini akadinda akisema ni wakati wa kufunga na kuomba. Kwa mujibu wa baadhi ya jamaa wa familia za walioathirika, kanisa hilo huwataka watoto kuanza kufunga hadi kufariki, kisha wanafuatwa na kina mama na mwisho wanaume.


Chanzo: TUKO.co.ke 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo