Kocha Ruvu Shooting afungiwa kwa kuwatukana Azam TV


Kocha msaidizi wa Klabu ya Ruvu Shooting, Renatus Shija ametozwa faini ya TZS milioni moja kwa kosa la kukataa kufanya mahojiano na mtangazaji wa televisheni ya mdhamini mwenye haki za matangazo ya televisheni, Azam TV.


Taarifa hiyo imetolewa na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB)  baada ya kikao kilichofanyika Aprili 15, 2023 ili kupitia mwenendo na matukio mbalimbali ya ligi na kufanyia maamuzi.


Kamati imesema kocha huyo alikataa mahojiano baada ya kumalizika kwa mechi ya Tanzania Prison waliofunga magoli 3-1 dhidi ya Ruvu Shooting.

Kocha Renatus amefungiwa michezo mitatu na kutozwa mfaini ya TZS milioni moja kwa kosa la kuwatolea lugha ya matusi wafanyakazi wa Azam TV ambao walikuwa wakijaribu kumsihi akubali kufanya mahojiano hayo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo