Aliyemuua Mumewe Sababu ya shamba Auawa na Mwanawe Kutokana na Shamba Hilo hilo

Mwanaume mwenye umri wa miaka 26, anadaiwa kumuua mama yake katika kijiji cha Migosi nchini Kenya kutokana na mzozo wa ardhi kabla ya kujisalimisha kwa polisi.


Kabla ya kujisalimisha katika kituo cha polisi cha Sinaga, mshukiwa, Silas Oduor Odongo, anadaiwa kumuua mama yake Jenifer Atieno. Mshukiwa huyo alizozana kwa muda mrefu na mamake akitaka kumfurusha kutoka kwa mali aliyodai ni yake, kulingana na Franklin Odhiambo, chifu msaidizi wa eneo hilo. 

Aliambia Radio Ramogi kwamba mzozo huo ulianza mwaka wa 2004 kuhusu kipande hicho cha ardhi wakati marehemu, Jenifer Atieno, alishtakiwa kwa kumuua mumewe.


Chifu huyo anadai kuwa marehemu alihukumiwa kifungo cha muda gerezani kwa madai ya kumuua mumewe kutokana na kipande cha hicho cha ardhi ambacho walikusudia kujenga nyumba. 

Odhiambo alidai kuwa marehemu Jenifer Atieno aliamua kujenga nyumba yake katika eneo tofauti baada ya kumaliza kifungo chake gerezani kabla ya mwanawe Silas Oduor kudai umiliki wa shamba hilo hilo. 

Chifu huyo Msaidizi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo akisema kuwa Atieno na mwanawe hawakuwa wakipatana uso kwa uso kwa muda kabla ya jana asubuhi ambapo inadaiwa alimkatakata na kumuua. 

Alidai kuwa huku mshukiwa anapozuiliwa na polisi, uchunguzi unaendelea na mwili wa marehemu ulikuwa umesafirishwa hadi katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya rufaa ya kaunti ya Siaya.

Chanzo: TUKO.co.ke 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo