Rwamlaza acharuka wabunge waliotimka Chadema kuitwa Covid-19

 
Mbunge wa Viti Maalumu, Conschesta Rwamlaza amesema wanaowabeza wabunge 19 na kuwaita Covid-19 hasa wanapompongeza Rais Samia Suluhu Hassan, ni kwa sababu hawataki kukubali ukweli wa kazi yake.


Rwamlaza ametoa kauli hiyo Jumatatu Aprili 17,2023 wakati akichangia kwenye hotuba ya Makadirio na Mapato ya Wizara ya Tamisemi kwa mwaka 2023/2024 ambapo amesema wabunge 19 wako kwa ajili ya kuwasimamia na kuwasaidia Watanzania.

Mbunge huyo amesema kwenye ukweli wataendelea kusema kuusema bila kuogopa kwasababu wanatambua kazi kubwa inayofanywa na Rais Samia.

Mbunge huyo ni miongoni mwa wabunge 19 wa Chadema ambao wamekuwa kwenye mzozo na chama chao na tayari wamepelekana mahakamani wakidaiwa kuwa waliingia bungeni kinyume na sheria na utaratibu wa chama chao.

“Sisi wanatuita Covid-19, sawa lakini nataka kuwaambia kuwa ‘we are women at work’ (Wanawake tuko kazini) na kwamba tunakwenda na mama lakini kama kuna mwanaume atafanya kazi nzuri tutampongeza tu,” amesema Rwamlaza.

Mbunge huyo amemtaja Rais Samia kwamba aliwaita wanawake na kuwaambia kuhusu wanawake kushikamana kazi ambayo wataendelea kuifanya wakati wote.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo