Polisi yamuita kituoni dereva aliyepigwa na trafiki

 


Jeshi la Polisi mkoani Morogoro, limemtaka dereva aliyeonekana kwenye video mtandaoni akigombana na askari Polisi watatu Kitengo cha usalama barabarani afike kituo cha Polisi ili aleleze tukio hilo lilivyokuwa pamoja na Madhara aliyopata kutokana na tukio hilo.


Wito huo umetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama wakati akitoa ufafanuzi wa tukio hilo ambapo amesema tayari askari hao wamehamishwa vitengo na kupangiwa kazi nyingine huku hatua zingine za kijeshi zikiendelea.

RPC Mkama amesema baada ya askari hao kuhamishwa vitengo vya kazi wamemtaka dereva ambaye aliyeonekana akigombana na askari hao kufika kituo ili kueleza undani wa tukio hilo.

Hata hivyo kamanda Mkama hakuwataja kwa majina askari hao wala eneo iliporekodiwa tukio lakini amekiri ni kweli limetokea ndani ya mkoa wa Morogoro huku sauti za video zilisikika wakitaja kua eneo hilo ni Mikese barabara ya Morogoro – Dar es Salaam.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo