Mnyeti ashtakiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka


Mbunge wa jimbo la Misungwi Mkoani Mwanza, Alexander Mnyeti amesomewa mashtaka ya matumizi mabaya ya madaraka akiwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara.


Hata hivyo, Mnyeti hakuwepo mahakamani wakati kesi yake iliposomwa mjini Babati jana Februari 7, 2023 dhidi ya Kampuni ya Uwindaji ya HSK Safaris Ltd ya Wilaya ya Simajiro, kwa kosa la matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia hasara kampuni hiyo.

Wakili wake Kuwengwa Ndojekwa ambaye aliiomba mahakama mbele ya Jaji Mfawidhi, John Kahyoza imruhusu aiunganishe serikali kwenye kesi kwa sababu yale anayotuhumiwa kuyatenda yalitendeka akiwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara na alikuwa mtumishi wa umma.

Mnyeti anadaiwa kushirikiana na Ofisa Mtendaji wa Kata ya Emboreet, Belinda Sumari na Salehe Alamry kuinyanganya kitalu cha uwindaji Kampuni ya HSK Safaris Ltd bila kufuata sheria.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo