Naibu Waziri Mahundi akiri kupokea Maagizo ya CCM

Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) amepokea maagizo ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Daniel Chongolo aliyayatoa katika ziara yake ya siku tisa Mkoani Morogoro ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 46 ya CCM.


Mahundi amesema Mkoa wa Morogoro umepokea jumla ya shilingi bilioni 72 za miradi ya Maji zilizotolewa na serikali inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye ana dhamira ya kumtua mama ndoo kichwani.


Aidha ushirikiano baina yake na Waziri wa Maji Jumaa Aweso na watendaji wa wizara ya Maji watahakikisha miradi yote inayotekelezwa inakamilika mwezi juni,2023.
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo