Mchungaji Awasuta Watu Wanaochinja Kuku Kusherehekea Krismasi

Kuku ndiyo mlo unaopendelewa zaidi siku ya Krismasi na familia za Kiafrika.


Hapana shaka kuwa watu wengi huchinja kuku kila Desemba 25, ili kusherehekea Krismasi lakini kulingana naye na mchungaji Ezekiel Odero sio lazima.


Akizungumza wakati wa ibada kanisani, mtumishi iuyo wa Mungu aliwakanya watu kuchinja kuku kwa sababu ya sherehe ya Krismasi. Mhubiri huyo alidai kwamba sherehe za Krismasi zinapaswa kuachiwa watoto pekee, akiongeza kuwa watu wazima wanapaswa kufanya kazi siku hiyo badala ya kusherehekea.


"Mimi nakuuliza swali moja tu mtu wa Mungu. Leo umefunga kuku wala kesho, kwani wewe ni mtoto? Ni mara yako ya kwanza mpaka uikule Disemba 25? Kwa nini usipumzike? Kuwa mtu mzima. Lisha watoto lakini lisha roho. Jiulize, nimekuwa kwa this celebration miaka yote sherehe hii imebadilisha maisha yangu vipi?" “Unapotumia muda kusherehekea baadhi ya watu wanafanya kazi na watafanikiwa zaidi,” Ezekiel alisema.


Kando na hayo, inakumbukwa kuwa Ezekiel aliwaonya watu hususan kutoka jamii ya Wajaluo, kutotumia pesa nyingi katika mazishi ya wapendwa wao. Mtumishi huyo wa Mungu alisema kuwa katika jamii ya Wajaluo, watu hununua majeneza ya bei ghali na kujenga makaburi ya kifahari ili kuwazika wapendwa wao, jambo ambalo kwa mujibu wa mhubiri huyo, sii la lazima. 


“Nakuonya ukipamba mazishi unaifanya roho ya kifo ipende nyumba yako, jinsi unavyopamba mazishi ndivyo unavyoifanya roho ya mauti kusherehekea, itachukua mtu mwingine na sio mtu asiyefaa kitu bali msomi.Ndiyo maana ukienda kwa Wajaluo, utakuta kaburi la profesa, daktari.Watu muhimu hao," Ezekiel alisema. 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo