Walimu watakiwa kupunguza matumizi ya viboko

Rai imetolewa kwa walimu wote wa shule za msingi na sekondari na vyuo nchini kupunguza matumizi ya viboko na vitisho kwa wanafunzi kama njia ya kufanya wafaulu katika masomo yao kwa kuwa huo si mtazamo sahihi.


Rai hiyo imetolewa Jijini Dar es Salaam na Kamishna wa Elimu, Dkt. Lyabwene Mtahabwa wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa siku mbili wa wadau wa Mradi wa Kuendeleza Elimu ya Ualimu (TESP) ambapo alimwakilisha Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Francis Michael

Ameongeza kuwa walimu wanatakiwa wafahamu kuwa watoto wote hawana uwezo unaofanana hivyo wanatakiwa kuwachukulia watafute mbinu mbalimbali za kumsaidia kila mmoja.

“Maendeleo ya kweli katika nchi huletwa na elimu bora, elimu bora huletwa na walimu bora na walimu bora sifa yao kuu ni upendo kwa wanafunzi na wadau wengine wa elimu. Mwalimu ni kioo cha jamii, amejaa hekima na busara na ni kimbilio la watu wote,” amesema Dkt. Mtahabwa.

Amesema lengo la mkutano huo ni kutafakari namna ambavyo mradi umekuwa ukitekelezwa na kujadili jinsi ya kuimarisha na kuendeleza mambo yaliyotekelezwa kwa mafanikio baada ya mradi kuisha.

“Kwa hiyo siku hizi mbili tutaangalia nini kimefanyika kupitia Mradi huu wa TESP na kisha kuweka mikakati ya namna ya kuendeleza mradi huu,” ameongeza Dkt. Lyabwene.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo