Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa alikuwa miongoni mwa maelfu ya waombolezaji waliofika katika ibada ya kuaga mwili wa Balozi, Fulgence Kazaura aliyefariki dunia mwishoni mwa wiki akiwa katika matibabu nchini India.
Ibada hiyo ilifanyika katika Kanisa Katoliki la Mt
Peter, Oysterbay jijini, na kuhudhuriwa na viongozi wa chama na
Serikali, mabalozi mbalimbali Tanzania waliokuwa wanafanyakazi nje ya
nchi kupitia Chama cha Mabalozi Wastaafu (ACTA), wakurugenzi, wanazuoni
na wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Akizungumza wakati wa ibada hiyo, mtoto wa
marehemu, Kamugisha alisema kuwa baba yao alifariki kutokana na ugonjwa
wa saratani ya koo ambayo ilianza kumsumbua tangu mwaka 2012 na
iligundulika Juni mwaka jana.
Alisema kuwa baba yao alikuwa akilalamika
kushindwa kumeza chakula na baada ya kuhangaika na matibabu katika
hospitali mbalimbali nchini, Juni mwaka jana walimpeleka nchini India
alikobainika kusumbuliwa na ugonjwa huo.
“Walimtibia na alikuwa anaelekea kupata nafuu
kwani walau alirejea katika hali ya kawaida ingawa siyo kama awali”
alisema na kuongeza kuwa ilipofika Agosti hali ikabadilika ikabidi
wamsafirishe tena nchini India ambako alitibiwa kwa miezi miwili kisha
kurudi nchini.
Alisema hali ilibadilika tena Oktoba mwaka jana
ndipo akarudishwa nchini India ambako walimfanyia uchunguzi na
kugundulika kuwa saratani ilikuwa imesambaa sehemu zingine.
Kwa mujibu wa ratiba ya maziko, mwili wa marehemu
utaagwa leo kwenye Ukumbi wa Nkrumah wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(UDSM), kabla ya kusafirishwa kwenda kijiji alichozaliwa cha Igurukati,
Bugandika mkoani Kagera kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika Jumamosi.
Kabla ya umauti, Balozi Kazaura aliyezaliwa 11
Septemba,a 1940, alishika nyadhifa mbalimbali kama Ukatibu Mkuu wizara
mbalimbali na kuwa balozi wa Tanzania Ulaya (EEC).

Viongozi
wa Kanisa hilo la Mt. Peter wakiwaongoza waomboleazaji kuaga Mwili wa
aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Marehemu Balozi
Fulgence Kazaura aliefariki Dunia juzi huko nchini India alikokwenda kwa
ajili ya Matibabu.

Rais
Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh. Benjamin Mkapa akiwaongoza waomboleazaji
mbali mbali kutoa heshima za mwisho wakati wa kuaga Mwili wa aliyekuwa
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Marehemu Balozi Fulgence
Kazaura aliefariki Dunia juzi huko nchini India alikokwenda kwa ajili ya
Matibabu

Waziri
Mkuu Mstaafu,Jaji Joseph Warioba akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa
aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Marehemu Balozi
Fulgence Kazaura aliefariki Dunia juzi huko nchini India alikokwenda kwa
ajili ya Matibabu.

Kaimu
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM),Prof. Rwekaza Mkandala
(mbele) Sir George Kahama,pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara,Mzee
Phillip Mangula wakitoa heshima zao za Mwisho kwa Mwili wa aliyekuwa
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Marehemu Balozi Fulgence
Kazaura aliefariki Dunia juzi huko nchini India alikokwenda kwa ajili ya
Matibabu

Rais
Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh. Benjamin Mkapa akimfariji Mjane wa Marehemu
pamoja na watoto wakati wa Ibada maalum ya kuaga Mwili wa aliyekuwa
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Marehemu Balozi Fulgence
Kazaura,.

Waziri Mkuu Mstaafu,Jaji Joseph Warioba akiifariji familia ya Marehemu Balozi Fulgence Kazaura.

Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara,Mzee Phillip Mangula akiifariji familia ya Marehemu Balozi Fulgence Kazaura.
