Tazama hapa Uone Uzuri wa Makete

Hifadhi ya taifa ya pori la akiba la Mpanga Kipengele, Ilianzishwa mwaka 2002 ikiwa ndani ya wilaya tatu wilaya hizo ni Wanging'ombe, Makete na Mbarali, na ikipatikana ndani ya mikoa miwili mkoa wa Njombe na mkoa wa Mbeya.


Katika hifadhi hii yanapatikana maporomoko ya maji maarufu "Kimani Water falls ambayo yapo Wilayani Makete.


Maporomoko haya yana urefu wa mita 2002 ndiyo maporomoko yenye kuvutia kutokana na muonekano wake yakiwa na Bwawa la mapenzi ndani yake.


Mbali ya kuwa na bwawa la Mapenzi kunapatikana pia mabwawa mengine Asili ya kuogelea (Natural swiming pools) ambayo yamejitengeneza, wageni mbalimbali huyatumia kuogelea bila ya kikwazo chochote.


Lakini maporomoko ya mto Kimani ndiyo husafirisha maji na kuyapeleka katika mito mikubwa kama vile Mto Ruaha mkuu (The Great Ruaha River).


Katika maporomoko hayo pia inapatikana njia aliyokuwa akiitumia Chief Mkwawa kwenda katika pango ambalo alikuwa akiishi kujificha na kuangalia ulinzi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo