Mtoto afariki dunia baada ya Kufanyiwa Tohara


Familia moja kutoka eneo la Tarakwa, Uasin Gishu, inaomboleza kifo cha mwanao mwenye umri wa miaka 14.


Baba yake mvulana huyo, Gilbert Kirwa Maina alieleza kuwa mwanawe, Ibrahim Kirwa alifariki dunia baada ya kufanyiwa tohara ya kitamaduni mnamo Jumamosi, Desemba 3,2022 "Niombee mimi na familia yangu. Nilimpoteza mwanangu mpendwa Ibrahim Kirwa mnamo tarehe 22 Disemba katika ICU Mtrh kufuatia maambukizi makali baada ya tohara," aliandika kwenye Facebook. 


Baba huyo alieleza kuwa furaha ya mwanawe kuhitimu kuwa mwanamume kamili ilikatizwa ghafla baada ya shughuli hiyo kugeuka kuwa chungu huku miguu yake ikianza kuvimba, kuwa na maumivu ya kifua na tumbo kujaa.


Maina aliambia Nation kwamba mwanawe alipatikana na mshtuko siku 18 baada ya sherehe ya kutoka jandoni. "Siku kumi na nane baada ya kutairiwa, na baada ya matibabu kadhaa, hali yake ilizidi kuwa mbaya, na hivyo kulazimu kumpeleka kwa matibabu maalum katika hospitali ya Eldoret. Kwa kuwa alikuwa na hali mbaya, alilazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) baada ya aligundulika kuwa na mshtuko,” alisema. 


Ibrahim alikuwa amemaliza tu Mtihani wa Kitaifa wa Darasa la Nane (KCPE) wa 2022 na kupata alama 395. "Alifariki siku tatu baadaye akiwa bado anaendelea na matibabu. Warika wengine wanne waliotairiwa naye walikuwa na afya njema na walihitimu Disemba 28," aliongeza. Kirwa sasa anatoa wito kwa wazazi kote nchini kuwa makini dhidi ya mila na desturi hiyo ya kizamani ambayo inaonekana kuwa imepitwa na wakati. Aliwashauri walezi kuwa wepesi kuwakimbiza watoto wao kupata matibabu kila wanapopata dalili hizo ili kuepuka kupoteza maisha.


"Watoto wengi mkoani hapa sasa wametengwa na maradhi kama haya yanaweza kutokea, wanapaswa kuwakimbiza watoto wao hospitalini bila kusita ili kuepusha kupoteza maisha," alisema baba huyo mwenye huzuni. Mjomba wa marehemu, John Birech, alisema wengi katika familia walikuwa na dhana kwamba mabadiliko ya hali ya hewa na lishe ilisababisha hali hiyo kabla ya kuwa mbaya zaidi.


Chanzo: TUKO.co.ke 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo