Polisi yaonya kutojitangazia ushindi kabla ya matokeo

Polisi mkoani Shinyanga imewaonya wafuasi wa vyama vya siasa ambao wamekuwa wakijitangazia ushindi mapema kabla ya uchaguzi kufanyika, hali ambayo imekuwa ikionyesha kuwapo kwa viashiria vya uvunjifu wa amani siku ya kupiga kura endapo matarajio yao ya matokeo yakakwenda tofauti.
 
Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga, Justus Kamugisha, alitoa onyo hilo katika kikao cha wadau cha kujadili namna ya kudumisha amani siku ya uchaguzi Oktoba 25, mwaka huu kilichoandaliwa na shirika la Save the children mkoani hapa.
 
Kamugisha alisema anasikitishwa na baadhi ya wafuasi wa vyama vya siasa kuanza kujitangazia ushindi mapema kwa wagombea wao kuwa wao ndiyo wameibuka kidedea hata  kabla upigaji kura kutofanyika, kitendo ambacho aliomba kikome.
 
Hata hivyo, Kamugisha aliwaasa viongozi wa vyama hivyo vya siasa na asasi za kiraia zielekeze nguvu zaidi kutoa elimu ya upigaji kura, kuhesabu na kutangazwa kwa matokeo kwa muda huu mchache uliosalia ili wananchi wafahamu ni mtu gani anayestahili kutangaza matokeo ya uchaguzi. 
 
Naye Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Allynasoro Rufunga, akizungumza katika kikao hicho, alilaani kusikia baadhi ya wafuasi wa vyama vya siasa wamepanga kufanya vurugu siku ya uchaguzi endapo matarajio yao ya matokeo yatakwenda tofauti na kuwaasa wakumbuke kuna maisha mara baada ya uchaguzi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo