NA HALIMA KHOYA, MBEYA.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera ameliagiza Jeshi la Polisi Mkoani humo kuendeleo kumshikilia mchungaji anaye tuhumiwa kunajisi watoto nane wakazi wa mtaa wa Viwandani Kata ya Mwakibete Jijini Mbeya.
Homera ametoa maagizo hayo baada ya kupata taarifa hiyo kutoka Kwa mwenyekiti wa mtaa wa Viwandani Ndongole Mwatebela, ya kubaini uwepo wa mchungaji anaye najisi watoto katika mtaa huo kwa kuwarubuni kwa pipi na biskuti ambaye walifanikiwa kumkamata.