Mzee mwenye wake 7 aeleza anavyopata Raha

Andrew Ouma, mwanamume Mluo kutoka Kisumu, amefichua kwamba anaishi kwa amani na wake zake saba, akisema alioa mke wa kwanza akiwa na miaka 18 mwaka wa 1966.


"Baada ya miaka 11, nilioa mke wa pili, kisha baada ya miaka saba, nilipata mke wa tatu, na nikazidi kuoa hadi kufikisha mke wa saba," Ouma alisema kwenye mahojiano na Afrimax English.

Ouma ana watoto 30, wajukuu 16 na vitukuu watatu. Mwanamume huyo alidai kwamba sababu ya kuwa na wake wengi ni kwa minajili ya kumuenzi mama yake mzazi.


"Nimeoa wake wengi kwa sababu ni sehemu ya tamaduni zetu na pia unanifanya nikamilike," Ouma alisema.

Ouma halikadhalika alisema kwamba wake zake walikuwa ni majirani, na mama yake aliidhinisha awaoe. Mwanamume huyo wa miaka 77 amedai kwamba tayari amewajengea wake zake wanne nyumba, na kwa sasa anwajengea nyumba wake zake wengine watatu. Ouma pia amesema amewazawadi kila mmoja wao kipande cha ardhi.

Ouma amnesimulia jinsi alivyolelewa kwenye familia ambako baba yake alioa wake wengi, huku mamake akiwa mke wa sita. Mwanamume huyo aliongeza kusema kwamba yeye hukashifiwa mara kwa mara, ila hayo hayamjalishi kamwe.

Chanzo: TUKO.co.ke


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo