CHADEMA kuzuia mkutano mkuu wa CCM unaotarajia kufanyika 23 Julai

Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kimesema hakitarusu Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama cha Mapinduzi unaotarajia kufanyika tarehe 23 Julai mwaka huu kwa ajili ya kumkabidhi uongozi Mwenyekiti wa chama hicho Dk John Pombe Magufuli kutokana na Jeshi la Polisi kutumia nguvu kutawanya mikutano ya chama hicho na kuzuia mahafali ya wanafunzi wa vyuo vikuu.

Katibu Mkuu wa Baraza la vijana Chadema taifa Bw.Julius Mwita ameyasema hayo baada ya Jeshi la Polisi kuzuia mahafali ya kuwatunuku vyeti wanachama wa vyuo vikuu mkoani Kilimanjaro.
 
Amesema kitendo kinachofanywa na Jeshi la Polisi kutumia nguvu kuzuia mikutano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ni kukandamiza Demokrasia hapa nchini na kuwataka vijana kutokata  tamaa.
 
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Taifa (Zanzibar) Salum Mwalimu amesema wanasikitishwa na kitendo kinachofanywa na Jeshi la Polisi kutumia nguvu kutawanya mikutano ya chama hicho hapa nchini.
 
Akielezea mazingira ya kuzingirwa na Jeshi la Polisi Mwenyekiti wa Bazara la vijana Chadema mkoa wa kilimanjaro Bw.Dikson Kibona amesema walishangaa kuwaona wakizingirwa huku wakipewa amri ya kutawanyika la sivyo watatawanyishwa kama hawatatii amri.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo