Klabu ya Geita Gold yenye maskani yake Mkoani Geita, imeachana na mshambuliaji wake George Mpole.
Taarifa za Geita Gold FC kuachana na Mpole zimethibitishwa na Mtendaji Msaidizi wa Klabu hiyo, ambapo Mshambuliaji huyo ameruhusiwa kucheza timu yoyote kutokana na kufika kikomo kwa mkataba wake katika Klabu hiyo, mnamo Desemba 7, 2022.
“Uongozi wa Klabu ya Geita Gold unakutaarifu rasmi ya kwamba mkataba wako wa ajira kati ya Klabu na wewe umemalizika rasmi leo baada ya pande zote mbili kukubaliana na uko huru kujiunga na Klabu yoyote kuanzia leo”, ameeleza Mtendaji Msaidizi kupitia taarifa iliyoandaliwa ya kuachana na Mshambuliaji huyo.
Geita Gold FC imemshukuru Mshambuliaji huyo kwa ushirikiano wake na kazi nzuri tangu asajiliwe ndani ya Klabu, pia Klabu hiyo imemtakia kila la kheri na maisha mema katika majukumu yake ya Soka katika Klabu nyingine.