Mwanamke mmoja alizua tafrani kwenye mitandao ya kijamii baada ya kufunguka kuhusu kumnasa mumewe kitandani na dadake siku nne baada ya harusi yao
Katika klipu ya TikTok yenye hisia kali aliyoshiriki, mwanamke huyo alisema ugunduzi huo wa kushtua ulimvunja moyo hadi akakaa hotelini kwa wiki moja bila kuoga au kutoka nje
Aliporudi kazini, mumewe na dadake walikuja kuomba msamaha. Baadaye angezuia nambari zao ili wasimpigie simu tena. Mwanamke huyo alisema pia alizuia nambari za simu za mama yake na mama mkwe kwa sababu walimtaka awasamehe wawwili hao.
Alisema baadaye alihamia kwenye nyumba ya rafiki yake wa dhati. Akikumnuka matukio hayo mwanamke huyo aliona kwamba si ajabu dada yake alivaa nguo nyeupe kwenye harusi yake.
Alisema baadaye alihamia kwenye nyumba ya rafiki yake wa dhati. Akikumnuka matukio hayo mwanamke huyo aliona kwamba si ajabu dada yake alivaa nguo nyeupe kwenye harusi yake.
Video yake ilipata zaidi ya maoni milioni 3.7 kufikia wakati wa kuchapisha ripoti hii.