Hofu iligeuka na kuwa mshangao wakati mwanamume aliyekuwa amelewa kupita kiasi kutoka eneo la Katozi eneo la Nakonde kutoa ripoti ya uwongo kuhusu ajali ya barabarani.
Kulingana na ripoti, Clive Mukuwa alipiga simu katika idara ya wazima moto akidai kulikuwa na ajali mbaya inayohitaji usaidizi wa haraka. Jinsi Mukuwa alivyokipotosha kikosi cha wazima moto Kulingana na ripoti ya Nkani, kikosi cha wazima moto hakikupoteza muda na kukimbia eneo la tukio huku ving’ora vikilia na taa za dharura zikiwaka.
Hata hivyo, walipofika, wahudumu wa dharura walikutana na jambo lisilotarajiwa na la ajabu kwani mpigaji simu mwenyewe aikuwa mlevi chakari huku kifuatana na rafiki yake mlevi sawa.
Walipomhoji Mukuwa kuhusu eneo la ajali iliyodhaniwa, alielekeza kidole kwa rafiki yake huku akisisitiza kuwa alikuwa amepoteza fahamu muda mfupi kabla ya simu hiyo kupigwa. Kamishna wa Polisi wa Mkoa wa Muchinga, Dennis Moola alisisitiza umuhimu wa tabia ya kuwajibika wakati wa kupiga simu za dharura.
Je Mukuwa atafunguliwa mashtaka gani? Moola alionya kupiga simu za dharura tu katika hali mbaya sana, kwanisimu za uwongo zinaweza kuvutia adhabu. Wakati huo huo, mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 48, ameshtakiwa na kutozwa faini ya Kenya shilingi 89 kwa kutoa taarifa ya uongo kwa idara ya wazimamoto.
Mukuwa alishtakiwa kwa tabia inayoweza kusababisha kuvuruga amani, alilipa faini ya kukiri kuwa na hatia, na ameachiliwa huru. Ikiwa itapelekwa mahakamani, mwenendo huo unaweza kuvutia kifungo rahisi cha hadi mwezi mmoja.